Home Habari za michezo SIMBA WATUMA VIGOGO KABLA YA KIKOSI

SIMBA WATUMA VIGOGO KABLA YA KIKOSI

Habari za Simba SC

Imefahamika kuwa baadhi ya vigogo wa Simba SC wametangulia nchini Misri kwa ajili ya kuweka mambo sawa na moto, kabla ya mchezo wa Mkondo wa Pili wa African Football League dhidi ya Al Ahly.

Miamba hiyo ilikutana jana katika mchezo Mkondo wa Kwanza uliopigwa jana Ijumaa (Oktoba 20), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kuambulia sare ya 2-2.

Simba SC wamepania kubeba asilimia kubwa ya vitu vyao kama walivyokuja navyo Ahly ingawa hata viongozi waliopo Misri tayari wameshafanikisha mahitaji kadhaa kuhakikisha timu inatua kishua.

Kitakwimu, Simba SC ndio klabu ya Tanzania na Afrika Mashariki yenye uzoefu mkubwa si tu na timu za Misri, bali majiji makubwa ya nchi hiyo kwani imecheza na kuweka kambi mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.

Simba SC ndiyo klabu pekee ya CECAFA inayoshiriki michuano hii ya timu nane, kigezo kikiwa ni ubora kwenye viwango pamoja na kuwa na ushiriki wa mara kwa mara kufikia hatua ya Robo Fainali.

Taarifa zinaeleza kuwa kikosi cha Simba SC na baadhi ya viongozi kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam leo Jumamosi (Oktoba 21) kuelekea Cairo Misri, tayari mwa maandalizi ya mchezo wa Mkondo wa Pili dhidi ya Al Ahly.

Katika mchezo huo utakaopigwa Jumanne (Oktoba 24) Simba SC itatakiwa kusaka ushindi wa aina yoyote ama sare ya 3-3 ili kutinga Nusu Fainali ya African Football League.

Ikitokea matokeo ya mchezo huo yanakuwa 2-2 timu hizo zitakwenda kwenye mikwaju ya Penati, ili kumsaka mshindi wa jumla atakaeendelea na michuano hiyo kwenye hatua ya Nusu Fainali.

SOMA NA HII  HIVI HILI LA CHE MALONE LIMEKAAJE KITAALAMU