Habari za Simba
Habari za michezo

MASTAA HAWA SIMBA, WYDAD KUUKOSA MCHEZO WA MARUDIANO KWA MKAPA

Staff Desk December 10, 2023 12:34 pm

Kiungo mkabaji wa simba Sadio kanoute na nahodha wa timu ya Wydad, Yahya Jabrane wataukosa mchezo wa marejeano wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi utakaochezwa Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kanoute na Jabrane wote wataukosa mchezo huo kwa sababu za kikanuni za kuwa na kadi tatu za njano.

Kanoute alipata kadi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas wakati Simba akicheza nyumbani, ya pili alipata kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy pindi Simba ilipocheza ugenini na kadi ya tatu ameipata leo kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca, Simbaa ikicheza ugenini huku Jabrane yeye akipata kadi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy, ya pili dhidi ya ASEC Mimosas na ya tatu ameipata leo dhidi ya Simba.

Hadi sasa katika msimamo wa kundi B CAFCL michezo mitatu waliyocheza namba moja ni ASEC Mimosas pointi 7, namba mbili ni Jwaneng Galaxy point 4, namba tatu ni Wydad point 3 huku simba akishika mkia akiwa na pointi 2 baada ya kupata sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

YANGA WABORESHA KIKOSI KAZI, WAMBA WATATU HAWA HAPA KUTUA JANGWANI TATIZO LA YANGA KWENYE LIGI YA CAFCL LIPO HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply