Habari za michezo

MANGUNGU AWAPA NENO MASHABIKI WA SIMBA BAADA YA USHINDI A JANA

Staff Desk December 16, 2023 10:53 am

Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema timu yao imepitia kipindi kigumu cha kukosa matokeo lakini sasa wameanza kuyapata hivyo mashabiki waiunge mkono timu.

Amesema mpira ni kama vile maisha ya kawaida ambapo kuna wakati mwanadamu hupitia nyakati ngumu hivyo hakuna sababu ya kukata tamaa.

“Tumepita kwenye mechi mama tano au sita bila kupata matokeo mazuri, lakini sasa timu imeimarika, wachezaji wanaelewana.Unajua wakati mwingine sisi mashabiki huwa tunachangia timu kuzidi kufanya vibaya kutokana na mapenzi yetu.

“Tunatakiwa hata kama tunakosoa vitu, tukosoe kwa staha sababu wakati mwingine tunazungumza maneno makali ambayo yanawafanya hata wachezaji watoke mchezoni,” alisema Mangungu.

Simba jana ilipata ushindi wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar baada ya kupita takriban mechi mbili za Ligi Kuu pasi na kupata ushindi.

Simba sasa imerejea nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na alama 22 wakizidiwa alama 2 na Yanga ambao wapo nafasi ya pili.

ISHU YA PENATI YA SIMBA KURUDIWA IPO HIVI GAMONDI PRESHA TUPU, BAADA YA WABONGO KUMGEUZIA KIBAO YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply