Home Habari za michezo WAKATI USAJILI UKIZIDI KUSHIKA….YAO KOUASSI AIBUKA NA HILI JIPYA YANGA….

WAKATI USAJILI UKIZIDI KUSHIKA….YAO KOUASSI AIBUKA NA HILI JIPYA YANGA….

Habari za Yanga SC

Beki wa pembeni kutoka nchini Ivory Coast anayeshika nafasi ya pili kwa asisti katika Ligi Kuu Bara, Yao Kouassi nyuma ya Kipre Junior wa Azam FC, ameanza kunogewa na sasa anasema anatamani kufanya makubwa zaidi kwenye ligi hiyo akiwa na kikosi cha Mabingwa watetezi Young Africans.

Yao ameasisti mabao matano na kufunga moja, akizidiwa na Kipre mwenye asisti sita akiwa ndiye kinara hadi ligi inasimama ikiwa zimeshachezwa jumla ya mechi 105 amesema kuwa, anataka kuvunja rekodi aliyoiweka msimu uliopita alipokuwa na klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Beki hiyo amesema wakati akiwa Asec alitoa asisti 12 msimu mzima, kitu anachoamini kama ataenda na kasi aliyoanza nayo katika Ligi Kuu Bara anaweza kuifikia mara msimu utakapomalizika akiwa na mechi 19 na kikosi hicho cha Young Africans kilichocheza mechi 11 hadi sasa ikishika nafasi ya pili na pointi 30 nyuma ya Azam FC.

“Nilipokuwa Asec niliasisti 12, lakini hapa nataka kuzifikia hizo au zaidi, kwani kwa jinsi timu yetu ilivyo naona bado nafasi ipo kwa kuwa ligi bado haijamalizika tukiwa duru la kwanza,” amesema Yao ambaye ndani ya msimu wake wa kwanza nchini amekubalika haraka na mashabiki.

“Mimi kufunga sio kitu muhimu sana kwangu lakini ikitokea nafasi nitafanya, ila kitu napenda ni kuasisti.”

SOMA NA HII  HATARI YANUKIA LIGI KUU....MMILIKI MPYA WA IHEFU HAJULIKANI TFF....ISHU NZIMA IMEKAA HIVI...