Home Habari za michezo UNAAMBIWA ‘MOVE’ YA OKRAH KWENDA YANGA KUMBE ILIANZIA HIVI….UKWELI WOTE HUU HAPA..

UNAAMBIWA ‘MOVE’ YA OKRAH KWENDA YANGA KUMBE ILIANZIA HIVI….UKWELI WOTE HUU HAPA..

Tetesi za usajili yanga leo

Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umesema ulimfuatilia winga wa Ghana, Augustine Okrah na kuona anafaa kwenye kikosi chao na hivyo kuamua kumsajili ili kukiongezea nguvu.

Young Africans imemsajili nyota huyo wa zamani wa watani zao Simba SC kwa kumpa mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kutambulishwa rasmi kesho Jumapili (Desemba 31) visiwani Zanzibar, wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan.

Nyota huyo tayari ameshawasili nchini na kujiunga na timu hiyo na atakuwa miongoni mwa wachezaji kwenye msafara wa timu hiyo ilitarajia kuondoka leo Jumamosi (Desemba 30) kuelekeza Zanzibar.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe, amesema usajili wanaoufanya ni wakuboresha kikosi chao kulingana na matakwa ya Kocha wao Miguel Gamondi na hata ujio wa Mghana huo umepitishwa na kocha wao huyo.

Amesema awali walipanga kumtambulisha mchezaji huyo jana Ijumaa (Desemba 29), lakini Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said ametaka akatambulishwe Zanzibar.

Kwa mantiki hiyo, Okrah sasa atatambulishwa katika mchezo wa kesho Jumapili (Desemba 31) dhidi ya Jamhuri.

“Huyu mhezaji ni mgeni lakini mwenyeji tunatarajia kumtambulisha katika mchezo wetu wa kwanza, utambulisho wake utafunika ile shoo ya msanii Diamond aliyoifanya pale uwanja wa Amaan, tunafanya usajili kwa mapendekezo na maagizo ya kocha wetu, alitaka tusajili winga, tumemfuatilia Okrah na kocha mwenyewe amefanya hivyo na ndio sababu ya kumsajili,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa timu hiyo ilitatarajia kuondoka leo Jumamosi (Desemba 30) kuelekea Zanzibar, huku wakiwa na dhamira ya kutwaa taji la ubingwa wa michuano hiyo na ndio sababu ya kwenda na kikosi kamili.

“Safari hii tumejipanga vizuri kwenda Zanzibar, tunaenda kuchukua ubingwa wa michuano hii, tumeshaona michezo minne mpaka jana, sasa sisi Young Africans tunaenda kuwafundisha soka,” amesema Kamwe.

Mbali na Okrah, Young Africans pia inatajwa kuwa kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumsajili nyota wao wa zamani Simon Msuva ambaye kwa sasa hana timu.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA:MUUNGANIKO KWELI BADO, SIWEZI KUDANGANYA