Home Habari za michezo SASA NI SIMBA NA REKODI HIZI ZA KIBABE KWA MKAPA

SASA NI SIMBA NA REKODI HIZI ZA KIBABE KWA MKAPA

Habari za Simba leo

Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0, dhidi ya Wydad Casablanca, Simba imefanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti.

Kwanza ndio imekuwa timu pekee kutoka Tanzania kumaliza kipindi cha kwanza cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa inaongoza msimu huu kwenye hatua ya makundi.

Vilevile imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kwenye michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo wa hatua ya makundi.

Pia kiungo mshambuliaji Andre Onana ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka timu ya Tanzania katika michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza.

Timu nyingine inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kutoka Tanzania ni Yanga, ambayo itacheza kesho na Medeama saa 10:00 kwenye Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  FEI TOTO HAKUNA KUPOA HUKO LIGI KUU