Home Habari za michezo VYUMA VIPYA YANGA HIVI HAPA….GAMONDI ATIA TIKI….ENG HERSI AANZA NA MCONGO HUYU…

VYUMA VIPYA YANGA HIVI HAPA….GAMONDI ATIA TIKI….ENG HERSI AANZA NA MCONGO HUYU…

Tetesi za Usajili Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amekabidhi ripoti na kutoa mapendekezo yake katika dirisha dogo la usajili anahitaji mchezaji mmoja tu nafasi ya ushambuliaji.

Miongoni mwa washambuliaji ambao wanatajwa ni Sankara Karamo wa Asec Mimosas (Ivory Coast) na Emmanuel Bola kutoka Lupopo ya DR Congo na Jonathan Sowah (Medeama FC-Ghana).

Taarifa za uhakika kuwa Bola aliamua kugomea kufuatia uamuzi wa klabu yake kuingia kwenye makubaliano na Yanga kwa ajili ya uwezekano wa kuhama, kwa hakika timu ya Tanzania, Yanga ilithibitisha kuwa ina nia ya mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho wa dola 100. 000.

Mtoa habari huyo amesema ripoti ya Kocha Gamondi inaonyesha kuwa, ana shida na mshambuliaji mmoja ambaye atakuja kuziba nafasi ya Fiston Mayele hadi sasa ipo wazi kwa kuhakikisha anakuja mtu sahihi na maeneo mengine yamekamilika.

“Tayari Gamondi alishawaambia aina ya mshambuliaji anayemuhitaji na kilichobakia kwa sasa ni kukamilisha masuala machache na baada ya hapo watamtambulisha Ili kujiunga mazoezini mapema kujiandaa na Michuano mbalimbali inayowakabili.

Katika ripoti ya usajili inaonyesha anataka mchezaji mmoja kwenye eneo la ushambuliaji. ametuambia maeneo mengine kwa sasa hayana shida yoyote na badala yake ameagiza ashushiwe straika mmoja mahiri wa kucheka na nyavu,” amesema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa “ kikosi chake hakina matatizo yoyote safu ya ulinzi na ile ya kiungo kwani wamesheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa na hata mawinga waliopo amesema kwa sasa wanamtosha isipokuwa anahitaji mtu wa kusaidiana na akina Kennedy Musonda pamoja na Clement Mzize,”.

Amesema mshambuliaji huyo anakuja kuchukua nafasi ya Hafiz Konkoni ambaye wenye timu yao wapo kwenye mazungumzo ya kumtafutia timu ili wamtoe kwa mkopo au ikibidi kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba naye.

“Huyo straika anakuja kuchukua nafasi ya Hafiz Konkoni ambaye kama sio kumtoa kwa mkopo tutasitisha kabisa mkataba naye tuachane kwa wema. Kocha Gamondi ametuambia usajili mkubwa utafanyika dirisha kubwa msimu utakapomalizika,” amesema.

Kuhusu taarifa za Simon Msuva, alikiri kwamba wanawasiliana naye lakini hakuna muafaka wowote kwani Gamondi hana shida sana na winga ila lolote linaweza kutokea kutokana na uzoefu mkubwa alionao nyota huyo.

kocha huyo kuhusu usajili safu ya ushambuliaji alisema. “ Kuna timu nyingi zinahitaji mshambuliaji, Madrid wanahitaji hata Barcelona wanae Lewandowski lakini bado wanahitaji mshambuliaji . Yanga inahitaji hata tukiongeza mmoja itabidi na yeye apewa muda na sio kuingia na kuanza kucheza mechi ya kwanza mnataka afunge mabao matatu,

Hapana kila mchezaji anahitaji muda kuzoea Ligi wakati mwingine tamaduni za nchi alizotoka na Tanzania ni tofauti kuna muda lugha inakuwa inampa shida wachezaji wengi sana .

Naye Ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe alithibitisha kuongeza mtu katika safu ya ushambuliaji na kudai ndani ya siku saba watamtambulisha nyota huyo.

SOMA NA HII  SIRI YA MAZOEZI MAGUMU YANGA HII HAPA....GAMONDI AOMBA MECHI YA HARAKA....