Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KWANZA AFCON….,FEI TOTO AIPA TAIFA STARS ‘ODDS ZA KWENDA’...

KUELEKEA MECHI YA KWANZA AFCON….,FEI TOTO AIPA TAIFA STARS ‘ODDS ZA KWENDA’ …

Habari za Michezo leo

Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka wazi kuwa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘AFCON 2023’.

Kiungo huyo ameongeza kuwa kwa sasa wanafanyia kazi kile ambacho wanaelekezwa na kocha wao kwa ajili ya kupata ushindi katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo ambayo watacheza na Morocco.

Stars imepangwa Kundi F la mashindano hayo likiwa na timu za Morocco, DR Congo na Zambia huku wakitarajia kucheza mechi yake ya kwanza keshokutwa Jumatano (Januari 17) dhidi ya Morocco.

Akizungumza kutoka katika kambi ya Stars nchini Ivory Coast yanapofanyika mashindano hayo, Feisal amesema: “Maandalizi yako vizuri na tunafuata maelekezo ya mwalimu.

Watanzania waendelee kutuombea dua tuweze kupata ushindi katika mchezo wetu ujao, naamini tutafanya vizuri na kupata ushindi mbele ya Morocco.

“Kuhusiana na wale ambao wanatuona sisi kama timu ndogo basi wajue kuwa mashindano haya hayana timu ndogo, wote ni timu kubwa na tutapambana kikubwa tukianza na mchezo huo na Morocco.

SOMA NA HII  UKISIKIA FUATA NYUKI ULE ASALI NDIO HII SASA......... AFL KIBOSI