Home Habari za michezo ENG HERSI USO KWA USO NA BOSI WA MBAPPE UFARANSA….WALICHOTETA HIKI HAPA…

ENG HERSI USO KWA USO NA BOSI WA MBAPPE UFARANSA….WALICHOTETA HIKI HAPA…

Habari za Yanga SC

Rais wa Klabu ya Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2024.

Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.

Habari za YangaVilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0

SOMA NA HII  MGUNDA: SIMBA SC TUMEFANYA MAKOSA ...TUMEADHIBIWA NA KAGERA..