Home kimataifa TANZIA: GERD MULLER NYOTA WA BAYERN AFARIKI

TANZIA: GERD MULLER NYOTA WA BAYERN AFARIKI


 NYOTA wa zamani wa Bayern Munich na Ujerumani, Gerd Mueller amefariki dunia leo hii akiwa na umri wa miaka 75


Muller ameaga dunia huku akiwa na rekodi kubwa kwenye maisha yake ya soka, ikiwemo mabao 566 kwenye mechi 607.


Mshambuliaji huyo kwenye timu yake ya taifa ya Ujerumani rekodi zinaonyesha kwamba alicheza jumla ya mechi 62 na alifunga mabao 68 ikiwa ni pamoja na lile la ushindi alilofunga katika Kombe la dunia 1974.

Alijiunga na Bayern Munich msimu wa 1964 alikuwa anaitwa jina la ‘Der Bomber’.

Muller alishinda kiatu cha ufungaji bora baada ya kutupia jumla ya mabao 10, 1970 kwenye Kombe la dunia na aliweka rekodi ya kufunga mabao 356 katika mechi 427 za Bundesliga na mabao 74 katika European katika miaka yake 15 ndani ya Bayern.

Alikuwa anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye kalenda baadaya kutupia jumla ya mabao 85 ilikuwa ni 1972 mpaka pale Lionel Messi alipoweza kuivunja rekodi hiyo 2021.

SOMA NA HII  ARSENAL YATAMBA KUREJEA KWENYE UBORA