Home Habari za michezo KISA TFF……SIMBA WAMLA ‘KICHWA’ KRAMO… ISHU YA NTIBAZONKIZA NI NUSU KWA NUSU…

KISA TFF……SIMBA WAMLA ‘KICHWA’ KRAMO… ISHU YA NTIBAZONKIZA NI NUSU KWA NUSU…

Habari za Simba leo

WAKATI Saido Ntibazonkiza akiendelea kuvutana na viongozi wa Simba juu ya kusaini mkataba mpya ili aendelee kuitumikia klabu hiyo, mabosi wamemchomoa kiungo mshambuliaji Aubin Kramo katika usajili wa ndani na ule wa kimataifa ili kukamilisha idadi ya nyota wa kigeni 12 wanaotakiwa kikanuni.

Awali ilielezwa Saido alikuwa afyekwe sambamba na Moses Phiri pamoja na Kramo kabla ya mambo kubadilika na kiungo huyo mshambuliaji kunusurika, badala yake Jean Baleke akarudishwa TP Mazembe na sasa mambo yamemgeukia Kramo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu akichomolewa mazima kikosini.

Kutolewa kwa Phiri na Baleke na kuingizwa kwa wachezaji watatu wa kigeni kumeifanya Simba kusaliwa na wachezaji 13, ndipo mabosi wakaamua kuzungumza na Kramo wakati wakimalizana na Saido ambaye mkataba wake umemalizika na walikuwa wakivutana juu ya kusaini mpya ili asalie Msimbazi.

Kwa mujibu wa kanuni ya Shirikisho la Soka Tanzani (TFF) inaruhusu wachezaji wa kigeni 12 kusajiliwa hivyo idadi iliyobaki inatakiwa kupunguza ndipo uongozi ulipoamua kufanya uamuzi wa kumuondoa Kramo kwenye usajili wa ndani na kumuacha kimataifa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa, Kramo ataendelea kuwa mchezaji wa Simba akiitumikia timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Ujio wa Freddy Michael, Pa Omar Jobe na Babacar Sarr umetufanya tufikie uamuzi huo ambao ni kutoka kwa kocha wetu. Amesema hatuwezi kumuacha Kramo kutokana na kukosa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kutokana na kupata majeraha,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika kutoka Simba.

Wachezaji wengine wa kigeni waliobaki kikosini ni Clatous Chama, Che Malone, Ayoub, Fabrice Ngoma, Henock Inonga, Luis Miquissone, Jobe, Fredy Michael, Babacar Sarr, Saido Ntibazonkiza, Sadio Kanoute na Willy Onana.

Hata hivyo wakati Simba ikitaka kumbakiza Kramo kwenye mechi za kimataifa, kwa mujibu wa kanuni za sasa mchezaji asiye kwenye usajili wa ndani hawezi kuitumikia mechi za kimataifa na hapo inalezwa mabosi wamekubaliana na mchezaji huyo wamlipe kila kitu, lakini akiwa hatumiki kwa kumchomoa kikosini jumla.

Kramo sio wa kwanza kukatwa usajili wa ndani ilishawahi kutokea miaka ya hivi karibuni kwa kiungo kutoka Kenya, Francis Kahata ambaye alimpisha Perfect Chikwende.

Uamuzi wa Simba kufanya hivyo ni baada ya kanuni za CAF kuruhusu wachezaji zaidi ya 12 wa kigeni kwenye michuano klabu. Dirisha la usajili kwenye michuano hiyo litafungwa Januari 31, mwaka huu.

Wakati Simba ikisema hayo habari za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zinasema timu inaweza kusajili mchezaji ila isimuombee leseni ya TFF, hivyo inawezekana Kramo akawa amebaki kwenye usajili kama mchezaji wa Simba lakini asiwemo kwenye mfumo wa TFF.

“Asipokuwepo kwenye mfumo wa TFF anakuwa hana leseni inayomuwezesha kucheza michuano yoyote ya TFF wala ya CAF kwani ili kucheza kimataifa lazima mchezaji awe na leseni aliyopewa na TFF;

“Kuna wakati Fifa na CAF walitoa kibali cha muda cha kuongeza wachezaji kwenye michuano ya kimataifa na kuruhusu mchezaji ambaye hana leseni ya shirikisho la nchi anayocheza, lakini akacheza michuano ya kimataifa kama ilivyotokea kwa Francis Kahata ambapo CAF na Fifa waliruhusu kwa sababu kulikuwa na ugonjwa wa Uviko-19,” kilisema chanzo hicho ambacho kilisisitiza kuwa lilikuwa ni suala la dharura la dunia na sasa halipo.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA KAMILI NA TEREHE KWA MECHI ZA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA...