Home Habari za michezo KUHUSU MCHAKATO WA MO DEWJI KUKABIDHIWA SIMBA….SERIKALI WAIBUKA NA HILI JIPYA…

KUHUSU MCHAKATO WA MO DEWJI KUKABIDHIWA SIMBA….SERIKALI WAIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi wamepokea barua kutoka kwa Baraza la Michezo Taifa (BMT) kuendelea na mchakato wa mabadiliko ya katiba ya maboresho ya Simba wanatarajia kuidhinisha katika mkutano mkuu ambao utakaofanyika Jumapili hii.

Hivi karibuni Simba waliteuwa kamati ya watu watano ikiongozwa na Mwenyekiti, Hussein Kitta kwa ajili ya mchakato wa mabadiliko ya katiba yake baada ya kupewa maelekezo na (BMT) kukosolewa na Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA).

Takriban miaka sita tangu klabu hiyo ilipitisha marekebisho ya katiba kwa ajili ya kubadili mundo wa umiliki na uongozi, ikakumbana na vikwazo kadhaa vilivyotokana na kanuni za sheria ya umiliki wa kampuni, kiasi cha Tume ya Ushindani (FCC) kuzuia kwa muda kuendelea na mchakato.

Kitta amesema Waziri mwenye dhamana ya muchezo aliitisha kikao kujadili kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba ya Simba, kukawa na mambo sita ambayo tayari yamefanyiwa kazi.

Mambo hayo ni mamlaka ya uteuzi ya bodi ya wadhamini baada ya kuteuliwa na sasa wanatakiwa kuchaguliwa katika mkutano mkuu, kuweka wazi nafasi ya kupatikana kwa Mwenyekiti, kuweka wazi malengo ya Katiba na kuyaweka wazi malengo ya mkutano

Kuwa na haja ya kuwa na kupitisha Kampuni ya inayoshiriki HISA za Simba Sport Club na kuweza wazi HISA asilimia 99 inashikiliwa na bodi ya wadhamini na asilimia moja kwa Mwenyekiti ambaye anatakiwa kuwa wazi kuwa ni wanachama

“Kutokana na mkutano huo [na waziri] bodi ya Simba ikaunda kamati hii. Tulipokea maoni mengi, mengine kwa barua pepe, mengine kwa barua, wengine kutupigia simu na kutumia ujumbe. Tulikaa vikao vinne kwa kati ya masaa 4-9.

“Lengo ni kukamilisha mabadiliko na serikali ilitupa muda ili kukamilisha jambo hili. BMT walisema kabla ya kupeleka kwa wanachama mlete hiyo rasimu tupitie kwanza. Baada ya vikao tukaenda BMT na nina furaha kuwambia kwamba tumepokea barua kutoka kwao ya kuridhishwa na yale tuliyopitisha.” amesema Kitta.

Ameongeza kuwa mambo sita yaliyopitishwa yana faida zaidi kwa mwanachama wa Simba kuliko kwa mtu mwingine yoyote, Faida ya jambo hili ni kwenda kukamilisha transformation.

“Ni wazi mabadiliko yatakwenda kutokea, jambo hilo tutawaachia CEO na bodi. Kazi yangu ni kuratibu maboresho ya vifungu, Katiba inataka wanachama kupata rasimu siku saba kabla ya mkutano mkuu na tayari tumeshawatumia.

Ushirikishwaji wa wanachama ulikuwepo na hata kamati ina wanachama ambao ni wenyeviti wa matawi lakini pia wito wa kuwataka wanachama kutoa maoni ulitolewa kupitia mitandao ya Simba.” Kitta.

SOMA NA HII  SIMBA vs AS VITA | GOMES - TUNAKUJA KIVINGINE