Home Habari za michezo KIGOGO YANGA ALIA MASHABIKI KUDHULUMIWA NA WACHEZAJI….ISHU IKO HIVI…

KIGOGO YANGA ALIA MASHABIKI KUDHULUMIWA NA WACHEZAJI….ISHU IKO HIVI…

Habari za michezo

Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Wakili Simon Patrick ameshangazwa na ba baadhi ya timu kupoteza muda wakati wa mchezo.

Hii ni baada ya Yanga kuambulia Sare dhidi ya Kagera na kushinda kwa mbinde mchezo wao uliofuata dhidi ya Dodoma Jiji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Simon ameandika; “Mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania wanadhurumiwa.

“Hakuna mpira wa miguu bila mashabiki, na kadri siku zinavyoenda mashabiki wa soka duniani wanadhurumiwa haki yao ya burudani.

“Haiwezekani mtu alipe kiingilio chake aingie uwanjani kuangalia mechi mwisho wa siku aishie kuona wachezaji wanalala tu uwanjani.

“Maskauti waliokuepo uwanjani jana kuwafatilia baadhi ya wachezaji, waliambulia kuona wachezaji hao wakilala tu, this is not fair at all.

“Wenye mpira wao FIFA wameona haya mambo mapema wameanzisha utaratibu wa “running time” yaani muda wote unaopotezwa utachezwa kwa dakika za nyongeza mpaka dakika 90 zitimie, ata kama ni kuongeza dakika 15 zitaongezwa.

“Huku kwetu mjini Tanzania mechi inacheza dakika 60, dakika zilizobaki ni za kulala, na hata zikiongeza hizo dakika za nyongeza hazichezwi zikaisha, hii sio haki kwa mashabiki wa soka.

“Muda umefika sasa bodi ya ligi kutoa semina kwa waamuzi wetu kuhusu hili suala la muda, tuige mambo mazuri kama tunataka kuendelea kupiga hatua. Football ni mchezo wa dakika 90. Play fair be positive”.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA MUKOKO KUTUA SIMBA...NABI AAMUA LIWALO NA LIWE...ADAI HAWEZI KUBADILI TIMU YAKE...