Home Habari za michezo HII HAPA THAMANI HALISII YA MKATABA WALIOSAINI YANGA JANA…..NI KUFRU TUPU…

HII HAPA THAMANI HALISII YA MKATABA WALIOSAINI YANGA JANA…..NI KUFRU TUPU…

Habari za Yanga leo

Klabu ya Young Africans, Jana Februari 22, 2024, imeingia ushirikiano wa kimkakati na Karimjee Group, ambao ni wasambazaji wa chapa ya pikipiki maarufu ya HERO.

Ushirikiano huu wa kibiashara kwa kipindi cha miezi 18, unakuwa ni wa mfano na wa kuvutia ambao Yanga SC na matawi yake kote nchini Tanzania watafanya kazi kama mtandao wa usambazaji wa pikipiki za HERO

Akizungumza wakati wa kuingia mkataba wa makubaliano hayo wenye thamani ya shilingi milioni 300, Rais wa Klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Said, ametaja faida za ushirikiano huo.

“Leo tumeingia makubaliano na Kampuni ya Karimjee kupitia Kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza. Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo. Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Yanga itapata kiasi cha Tsh 300m kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18.

“Mkataba huu unaruhusu kwa matawi yetu ya klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwa hiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakua kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero.

“Tuwahakikishie Kampuni ya Hero kuwa sisi ni klabu namba moja na tutahakikisha Hero ambao ni namba moja waendelee kubakia kuwa namba moja. Uwezo wa kuifanya Hero kuwa namba moja ni jukumu la kila mwanachama. Hivyo sasa bodaboda ni Hero,” alisema Eng. Hersi Said.

Kwa upande wa Nadah Dhiyeb ambaye ni Meneja Masoko Karimjee Mobility, alisema: “Tunajivunia kuingia mkataba na klabu yenye heshima kubwa sana katika historia ya soka la Tanzania. Tunajua muungano huu kupitia Matawi ya Yanga SC tutapanua wigo wa biashara yetu kwa kuweka mtandao mkubwa.”

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIGOMA KUHUSU GSM...BIASHARA UTD WASEMA WANACHOTAKA NI PESA TU..KMC MHHH...