Home Habari za michezo GAMONDI:- HII YANGA BADO SANA ….

GAMONDI:- HII YANGA BADO SANA ….

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema pamoja na kiwango bora cha nyota wake na matokeo mazuri waliyopata, lakini kama timu yenye malengo na ubingwa wanahitajì kuendelea kupambana hadi mwisho.

Akizungumza baada ya ushindi walioupata wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, Gamondi amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini vijana walipambana na kupata pointi tatu ambazo kwao ndio ilikuwa muhimu.

Amesema pamoja na matukio yaliyotawala likiwamo la kipa wake Metacha Mnata kuonyeshwa kadi nyekundu, hayakuwa muhimu na kikubwa ni pointi tatu na Yanga ina malengo hivyo lazima wachezaji wapambane kutetea taji lao.

“Mchezo ulikuwa mgumu, wapinzani walionekana nao kuhitaji ushindi lakini niwapongeze vijana kwa kupambana kuondoka na pointi tatu ambazo zilikuwa muhimu sana kwetu katika mipango ya kutetea taji letu msimu huu.”

“Amesema wanaenda kujipanga upya na mechi zinazofuata za mzunguko wa pili kwa kuangalia makosa, akieleza ishu ya Kenned Musonda aliyepangwa mapema kuanza mchezo wa jana kisha kutoonekana ni alipata changamoto ya kiafya na kufanya mabadiliko ya kumwanzisha Farid Mussa.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Prisons, Ahmad Ally amesema ameridhishwa na kiwango cha nyota wake japokuwa hesabu zao zilikuwa ni kushinda au kupata pointi moja, lakini Yanga walikuwa bora ukizingatia ukubwa wao na historia ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Amesema ikiwa mchezo wake wa kwanza kupoteza tangu atue kikosini humo, ameona sehemu ya mapungufu hivyo anaenda kusahihisha ili mechi ijayo dhidi ya Singida Fountain Gate wapate ushindi na kujiweka pazuri kwenye msimamo.

“Mimi niwapongeze wachezaji wangu kwa sababu walipambana na hii ni fursa kwao kujitangaza kucheza na timu bora iliyotoka kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, makosa yaliyoonekana tutayafanyia kazi kabla ya mchezo ujao,” amesema Ally.

SOMA NA HII  BODI YA LIGI YAZIPIGIA SALUTI SIMBA NA YANGA... WADHAMINI WAMWAGA MANOTI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here