Home Habari za michezo SAMATTA:- WATANZANIA SABABU YA TAIFA STARS KUFANYA VIBAYA KIMATAIFA…

SAMATTA:- WATANZANIA SABABU YA TAIFA STARS KUFANYA VIBAYA KIMATAIFA…

Habari za Michezo leo

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta amewataja Watanzania kama chanzo cha timu ya Taifa kufanya vibaya kwenye michuano mbalimbali.

Samatta ameweka wazi kuwa kuna mambo mengi ambayo yanasababishwa timu ya Taifa kutokufanya vizuri ikiwemo pia mifumo mibovu na Watanzania kuombea timu hiyo ifungwe.

“Kuna njia nyingi ambazo zinasababisha timu ya Taifa isifanye vizuri, kuna watanzania hata Stars ifungwe wao hawaumii na wengine wanaomba ifungwe kabisa”.

“Lazima tukubali sisi sio bora, na tuanze kutengeneza mfumo mpya ambao baada ya miaka kumi [10] au 15 tutapata timu ya Taifa ambayo ni Bora”.

“Tusidanganyane kwamba sisi ni bora kwasababu labda tuna Ligi bora, au Samatta yupo au tunaweza kununua wachezaji kwa bei kubwa Afrika”, amesema Mbwana Samatta.

Kwa upande mwingine mshambuliaji huyo wa klabu ya PAOK ya Ugiriki amesema kuwa kama nchi tunapaswa kuanza kuitengeneza timu ya Taifa upya kwa takribani miaka 10 hadi 15.

“Lazima tukubali kuwa kuna kosa tulilifanya mwanzo au hatukujiandaa kuwa sehemu fulani, tukubali na tuanze upya, tujenge upya”.

“Hii acha iendelee kuwepo lakini tuanze kutengeneza mfumo mpya na baada ya miaka 10 au 15 tutakuja kuwa na timu bora”, alisema Samatta.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA WAJICHIMBIA KANDA YA ZIWA