Home Habari za michezo STAILI YA KUZIBA MKONO YA MAXI INAMAANA GANI..? UKWELI USIOSEMWA HUU HAPA….

STAILI YA KUZIBA MKONO YA MAXI INAMAANA GANI..? UKWELI USIOSEMWA HUU HAPA….

Habari za Yanga leo

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa soka hasa Ligi Kuu Bara utaweza kukumbuka katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Dodoma Jiji baada ya mchezaji Maxi Nzengeli kufunga bao alishangilia kwa staili hiyo inayoonekana kwenye picha.

Lakini pia kama umekuwa ukifuatilia Fainali za AFCON zinazoendelea nchini Ivory Coast ambapo leo ndio fainali uliona staili ya Maxi ikitumika kwa wachezaji wa timu ya Taifa la DR Congo wakati wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya mchezo kuanza na hata pia wakifunga bao hufanya hivyo hivyo.

Pia leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons, Pacome Zouzoua baada ya kufunga bao la pili alitumia staili hiyo hiyo kushangilia bao licha ya kuwa yeye si raia wa Congo.

Kwani hii staili ina maana gani? Huenda ukawa unajiuliza.

Hii iko hivi; Wacongo wapo katika kampeni ya kutaka nchi yao kuwa na amani baada ya vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo huku wakiishutumu Rwanda kuwa ndio wachochochezi wa vita na kuwataka kuacha kuua raia wa Congo na kuiba rasilimali zao.

Wanatumia staili hiyo kuzitaka nchi za Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya kuacha kufumbia mdomo mauaji yanayoendelea na badala yake, wasaidie kupata suluhisho.

SOMA NA HII  MWAMUZI AFUNGUKA UTATA WA PENATI ZILIZOOKOLEWA NA ALLY SALIM DHIDI YA YANGA JUZI...