Home Azam FC KUELEKEA MECHI YAO NA SIMBA….KOCHA AZAM FC AANZA TAMBO ZA ‘KISENEGAL SENEGAL’….

KUELEKEA MECHI YAO NA SIMBA….KOCHA AZAM FC AANZA TAMBO ZA ‘KISENEGAL SENEGAL’….

Habari za Michezo leo

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouf Dabo amesema watautumia mchezo wao dhidi ya Simba SC kuonesha dhamira yao ya dhati ya kulihitaji taji la Ligi Kuu msimu huu.

Timu hizo zimepangwa kukutana Februari 9, 2024 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ukiwa mchezo wa kiporo baada ya ule wa awali kusogezwa mbele.

Akizungumza kocha huyo raia wa Senegal amesema uimara wa kikosi chake baada ya uboreshaji walioufanya kwenye dirisha dogo pamoja na muda mrefu wa maandalizi waliopata, ndivyo vinampa matumaini ya kushinda mchezo huo na kufufua matumaini yao ya kubeba taji hilo msimu huu.

“Kikosi changu kimezidi kuimarika kama ilivyokuwa kabla ya AFCON 2023 na kwa sasa tumeongeza ubora kutokana na maingizo mapya, hii inatupa nguvu ya kuifunga Simba SC Februari 9 na kuthibitisha ubora wetu na dhamira ya kubeba taji la Ligi Kuu msimu huu,” amesema Dabo.

Kocha huyo amesema anatambua hata wapinzani wao Simba SC nao kikosi chao kina mabadiliko makubwa kuanzia benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji, lakini hilo haliwapi presha sababu bado wanahitaji muda kujenga muunganiko tofauti na timu yake ambayo ipo tayari kwa mapambano.

Amesema wanataka kushinda mchezo huo kwa idadi kubwa ya mabao sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao kulingana na ukali wa safu yake ya ushambuliaji na upungufu waliokuwa nao wapinzani wao Simba SC.

Azam ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 ikikusanya pointi 31 katika mihezo 13 iliyocheza msimu huu, huku Simba SC wakiwa nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 23 katika mechi 10 ilizocheza.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO