Home Habari za michezo MANARA:- ‘TFF WANANIDHULUMU…..NILIMWAMBIA MO DEWJI SIWEZI KUKAA NA BARBARA…’

MANARA:- ‘TFF WANANIDHULUMU…..NILIMWAMBIA MO DEWJI SIWEZI KUKAA NA BARBARA…’

Habari za Michezo

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji S Manara amefunguka kuhusu sakata lake la kufungiwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kudaiwa kumtolea maneno machafu Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia.

Manara alifungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka miwili na faini ya Tsh milioni 10 tangu Julai 2022.

“Kwanza TFF wananidhulumu wao wanajua ,nchi inajua na kila mtu anajua lile tukio nilifanya mbele ya watu sikumtukana nimemwambia siondoki hili unanifanyia mara nyingi ,nilimjibu hivyo Karia ule ni mradi tu na mimi nakwambia nimefungiwa kwa sababu ya Simba “

“Hata ripoti yao inaeleza hakukuwa na matusi ,majibizano ndio umfungie mtu miaka miwili na milioni 20 ,mimi ni muungwana sijakukosea lakini nikaenda kumuomba radhi nyumbani kwake,” amesema Manara.

Aidha katika hatua nyingine,Haji Manara amesema kuwa baada kuteuliwa  barbara Gonzalez kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, yeye alimpigia simu Mohammed Dewji na kuomba aondoke.

Manara amesema alifanya hivyo kwa sababu alijua fika kuwa hatoweza kufanya kazi na dada huyo kutokana na tabia zake.

“Mo Dewji hana shida na mimi, mimi na yeye hatukuwahi kuwa na shida, kwanza Dewji anapenda watu wa aina yangu watu wanaoprotect timu lakini sasa wakawa wanamjaza kwamba Haji anakuwa maarufu kuliko wewe.

“Tukienda uwanjani mimi ninambwembwe na najua kujibrand siwezi kuingia uwanjani kabla uwanja haujajaa sasa ile wakawa wanamjaza kwamba wewe ndio unatoa hela lakini anasifiwa Haji, mimi nilimwambia hawa wanakujaza,” amesema Hajis Manara.

SOMA NA HII  MCHAKATO KOCHA MPYA SIMBA WAFIKIA PATAMU...KUTANGAZWA NDANI YA SIKU 14....SIRI YAFICHULIWA...