Home Habari za michezo SIKU 2 KABLA YA MECHI NA ASEC MIMOSA…FREDDY ‘ATINGISHA KIBUYU’ SIMBA…

SIKU 2 KABLA YA MECHI NA ASEC MIMOSA…FREDDY ‘ATINGISHA KIBUYU’ SIMBA…

Habari za Simba leo

Mshambuliaji Mpya wa Simba SC Freddy Michael Koublan amewatuliza mashabiki wa klabu hiyo kuhusu mchezo wa Mzunguuko watano wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Simba SC itacheza mchezo huo keshokutwa Ijumaa (Februari 23) katika Uwanja wa Felix Houphouet Bounie mjini Abidjan-Ivory Coast, huku ikihitaji ushindi ili kujiweka kaatika mazingira mazuri ya kufuzu Robo Fainali.

Freddy ambaye alisajiliwa Simba SC wakati wa Dirisha Dogo akitokea Green Eagles ya Zambia amewaambia Mashabiki na Wanachama wa Msimbazi kuwa anawafahamu Asec Mimosas vilivyo.

Amesema safari ya kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mechi hiyo kwake ni furaha kwani anaona kama ameanza vizuri michuano hiyo kutokana na kuwafahamu wapinzani wao.

Freddy ambaye hajawahi kuchezea ligi ya Ivory Coast, ameeleza imani yake ya kupata ushindi ni kubwa kwa sababu ya mambo makubwa mawili, nje na kikosi bora ambacho Simba SC wanacho kwa sasa.

“Mimi sio mgeni kabisa na ASEC nawajua na wananijua, kingine mazoezi tuliyofanya kabla ya safari hivyo vinanihakikishia kuanza kufunga mabao ugenini.

“Kitu kingine kinachonipa matumaini ya kushinda ni mechi nyingi za ligi tulizocheza kuliko wapinzani wetu hali iliyofanya miili yetu kuwa tayari zaidi kwa mashindano.

Muivory Coast huyo alitua Simba SC akiwa na rekodi ya kuifungia Green Eagles ya Zambia, mabao 12 katika mechi 17 alizocheza. Mechi tano za Ligi Kuu Tanzania Bara amecheza jumla ya dakika 199, amefunga bao moja.

Ikumbukwe Simba SC katika mechi tano za mwisho haijapoteza mchezo hata mmoja ukiachana na sare moja dhidi ya Azam FC, huku ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 36, katika mechi 15 ilizocheza.

ASEC ambao sasa iko kileleni mwa kundi na pointi 10 ikifuatiwa na Simba SC yenye alama tano, nayo imecheza mechi 15 za ligi ikishika nafasi ya nne ikiwa na Pointi 26, katika michezo minne ya mwisho imepoteza miwili na kushinda miwili akiwa katika uwanja wa nyumbani.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFAFANUA SABABU YA KUTOANZA NA NAMBA TISA DHIDI YA AL AHLY