Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA JWANENG JUZI…MASTAA SIMBA WAPEWA MTIHANI HUU MWINGINE…

BAADA YA KUMALIZANA NA JWANENG JUZI…MASTAA SIMBA WAPEWA MTIHANI HUU MWINGINE…

Habari ya Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amewataka wachezaji wake kuweka nguvu na akili zao kuelekea michezo yao minne ya mwezi Machi, kutafuta pointi 12 ili kujiweka vizuri kwenye kinyang’anyiro cha kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema kwa sasa anachoangalia zaidi kuona timu yake inaendelea kuwa na ubora ambao wamekuwa nao katika michezo miwili iliyopita na kufanikiwa kutafuta pointi hizo huku mechi tatu za nyumbani na moja ugenini.

Simba ina kibarua kigumu kutafuta pointi hizo Machi 6, 12 na 15, watacheza dhidi ya Tanzania Prisons, Singida Fountain Gate FC na Mashujaa FC mechi hizo watakazocheza nyumbani uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Machi 9, mwaka huu wataenda Mkwakwani, Tanga dhidi ya Coastal Union.

Benchikha amesema hawana muda wa kupoteza wanakibarua kigumu cha kuendelea kusaka pointi katika mechi za ligi kwa kufanikisha malengo yao ya kutaka kutwaa taji la ubingwa.

Amesema wamekuwa na ratiba ngumu tangu lakini wamefanikiwa kuvuna alama kwa ubora walionyesha mechi zilizopita kwenda kuonyesha katika mchezo unaofuata kusaka pointi katika michezo yao hiyo.

“Tumecheza vizuri sana katika michezo ya nyuma, ubora wa mechi ya juzi ulionyeshwa na wachezaji wangu naimani tutakuja kuona katika mechi zijazo na kuitumia michezo hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi robo fainali,” amesema Benchikha.

Ameongeza kuwa anafanya kazi hatua kwa hatua amemalizana na Jwaneng Gallaxy na kufanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa wanahitaji ligi kutafuta pointi 12.

Mshambuliaji wa Simba, Pa Omar Jobe amesema mpira ni kujiamini na kujiamini kile unachokifanya, matarajio yake kupambani timu ya Simba kufikia malengo ambayo yanatarajiwa.

“Mashabiki wanatakiwa kuniamiamini , nitapambana na kuendelea kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kushirikiana na wachezaji wenzangu kufikia kile ambacho kinatararajiwa na wanasimba,” amesema Jobe.

SOMA NA HII  KWA KOCHA MHISPANIA WA SIMBA...MKUDE, BOCCO NA AJIBU WASHINDWE WENYEWE TU...MRWANDA AWAPA NENO...