Home Habari za michezo ALIYEMPA CHAMA NGURUWE MWENYE MIMBA ATOA KAULI HII KWA MABOSI SIMBA….

ALIYEMPA CHAMA NGURUWE MWENYE MIMBA ATOA KAULI HII KWA MABOSI SIMBA….

Habari za Simba leo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe Project kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambaye ni shabiki kindakindaki wa Timu ya Simba SC Simon Mnkondya ametekeleza ahadi yake aliyoahidi endapo Simba ingepata magoli katika mechi yake dhidi ya timu ya Ihefu SC yenye maskani yake mkoani Singida.

Mkondya ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Kimataifa ya Kilimo cha Vanilla Duniani alitoa ahadi zawadi ya nguruwe mmoja mkubwa aina ya Large White mwenye kilo 500 sawa na shilingi Milioni 3 kwa kila goli ambalo lingefungwa na Simba SC katika mchezo wake na Ihefu SC wa Jumamosi Aprili 13, 2024 katika uwanja wa Iliti Singida.

Akizungumza na Vyombo vya habari jijini Arusha leo Jumapili Aprili 14,204 Mkondya amesema atatoa Nguruwe wa Shilingi Milioni tatu kwa mchezaji wa Simba SC aliyefunga goli pekee la penati katika mchezo wa Simba SC na timu ya Ihefu SC ya Mkoani Singida inavyofahamika sasa kama Singida Black Stars iliyotoka sare na Simba SC kwa kufungana bao moja kwa moja.

Amesema atauza Nguruwe 1,000 kwa lengo la kufanya usajili mkubwa kwa timu ya Simba hivyo viongozi wa Simba kwa sasa waanze mchakato wa kutafuta wachezaji wenye sifa ya kutumikia timu hiyo kwa msimu ujao kwa lengo la kupambania vikombe kwani timu ya Simba SC imepoteza mataji kwa misimu miwili na bado mwaka huu hawaoni matumaini ya kupata ubingwa wa ligi kuu.

Vile vile amemtaka mchezaji aliyefunga goli la kusawazisha la Simba SC dhidi ya timu ya Ihefu SC Clatous Chama kufika katika kijiji cha Nguruwe Zamahero Dodoma aweze kukabidhiwa nguruwe mwenye ujauzito ambaye ana thamani ya shilingi Milioni tatu.

SOMA NA HII  SIMBA KUMSAJILI KIPA HUYU KUTOKA KWA NABI