Home Habari za michezo SHABIKI:- KAMA SIO SERIKALI….MANGUNGU TUNGEMTUNDIKA MLIMA KILIMANJARO…

SHABIKI:- KAMA SIO SERIKALI….MANGUNGU TUNGEMTUNDIKA MLIMA KILIMANJARO…

Habari za Simba

Shabiki kindaki ndaki wa Klabu ya Simba, Mzee Saleh amesema kuwa mashabiki wa rimu hiyo wanaiogopa Serikali tu vinginevyo wangekuwa wameshafanya vurugu kwa viongozi wa Simba.

Mzee Saleh amesema hayo kuelekea mechi ya Dabi ya Yanga na Simba itakayopigwa Aprili 20, 2024 katika Dimba la Mkapa huku Simba ikionekana kuporomoka kiwango siku hadi siku baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu.

“Katika vitu vyote mimi naifikiria Aprili 20, Simba tukipigwa chache sana labda bao 5. Subiri maafa yanayokuja Aprili 20, tutatafutana kama mpira wa kona. Tena yatakuwa maafa makubwa mno.

“Kama watu hawajaenda kule Kigoma unadhani pale Lupaso watakuja (Uwanja wa Mkapa). Mashabiki wamechoka kila siku wanatoka wakiwa wameinamisha vichwa.

“Mashabiki wanachokiogopa ni Serikali vinginevyo hali ingekuwa si shwari ndani ya Simba. Endapo Serikali ingewaruhusu ‘fanyeni mnachotaka’, Mangungu mngemkuta amening’inizwa Mlima Kilimanjaro wameshasepa nae.

“Kama bado hatujamalizana na Azam mzunguko wa pili, uuwii basi kazi iko palepale hata nafasi ya pili tutaikosa,” amesema mzee Said.

SOMA NA HII  WAARABU WAINGIA MAZIMA MAZIMA KWA ONANA....KUTUMA OFA NONO KWA SIMBA KUMBEBA..