Hukumu ya shauri la mshambuliaji Mzimbabwe PRINCE DUBE wa Azam FC inatarajiwa kutolewa baada ya kusikilizwa .
Dube aliwakishwa na Wakili aliyeiwakilisha Yanga SC kwenye kesi ya Feisal Salum iliyofanana na hii, aliukana mkataba mpya wa Azam FC ambao unamuweka klabuni hapo mpaka Julai 2026, lakini alikiri kupokea pesa $110,000/ (Tshs 297M) ambazo zililipwa kwa mafungu ya $55,000/ (Tshs148.5M).
Alipoulizwa kuhusiana na pesa hizo kama anakumbuka kupokea na zilikuwa za nini, alisema anakumbuka na zilikuwa za bonasi. Kitu ambacho kiliwashangaza wajumbe kwani bonasi ilikuwa inazidi mshahara wake wa mwaka.
Bonasi zimeandikwa kwenye mkataba ambapo hazizidi $20,000/ (Tshs 54M) kwa mwaka. Madai ya Azam FC kwenye shauri hili yalikuwa kulipwa $550,000/ (Tshs 1.48b) hii ilikuwa inajumuisha buy out clause $300,000 (Tshs 810M) na nyingine ni gharama za kuchafuliwa.
Taarifa ambazo SOKA LA BONGO inazo ni kwamba atalipia kiasi cha mkataba uliopo sasa ambao ulikuwa hai kwa miezi isiyopungua 3, mkataba ambao thamani yake wakati unasainiwa ilikuwa
$100,000/(Tshs 270M), kwakuwa aliondoka kambini mkataba uko hai, atatozwa pesa kulipia hapo.
Lakini atarejesha $110,000(Tsh 297M) ya watu ambayo alikubali kupokea, pia atatozwa kiasi ingawa sio chote kutoka Buy-out clause ile ya $300,000, haijajulikana ila mpaka mahesabu yafanyike.
Kwa ujumla Dube atailipa Azam FC kiasi kisichopungua $200,000 lakini kisichozidi $300,000. Yani atalipa kisai kisichopungua Tshs 540M na kisichozidi Tshs 810M ili kuondoka Azam FC.
Kamati ilishindwa kujielekeza kwenye mkataba mpya wa Azam FC na Dube kwakuwa kulikuwa na mapungufu kwenye maeneo kadhaa, pia kuukubali ilikuwa kuhalalisha madai ya $550,000.
Kama kamati hii ingempa ushindi Dube ingejivua nguo kwakuwa ni Kamati hii hii pia ilimnyima haki Feisal Salum mara mbili ambaye alikuwa na madai kama ya Dube. Hukumu itatoka leo muda wowote.
Habari za ndani kutoka Azam FC zinasema wao wako tayari kupokea kiasi cha pesa kitakachoamuliwa na Kamati ila sio pungufu ya $300,000/ alidokeza kigogo mmoja. Uzoefu unaonyesha AzamFC hawapendi migogoro wanaweza kupokea hata $200,000/
SOMA NA HII KUHUSU FEI TOTO KUREJEA YANGA...STORI MPYA NI HII HAPA.....MUDA SI MREFU JAMBO LINAIVA..