Habari za Simba leo
Habari za michezo

EDO KUMWEMBE AWACHANA SIMBA…ADAI SIMBA KUMDHARAU RAIS YANGA…AMEFUNGUKA HAYA

Marce Ben Komba April 26, 2024 10:58 am

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe awechana klabu ya Simba akisema ni aibu kubwa kufurahia kufungwa bao chache na watani zao Yanga Sc.

Edo amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo cha bao 2-1 huku hofu yao ilikuwa ni kufungwa bao nyingi kama ilivyokuwa duru ya kwanza kutokana na ubovu qa kikosi chao.

“Sasa msimu umemalizika dhahiri kwa Simba. Sioni namna gani Simba wakichukua ubingwa kwa pengo la pointi lililopo. Baada ya Azam kucheza dakika 90 na za nyongeza dhidi ya Mashujaa bila ya kufunga bao lolote Ijumaa usiku sioni namna gani Yanga wanaweza kuzuiwa wasitwae ubingwa.

“Swali ni namna gani Simba watarudi msimu ujao. Wamejifunza kitu au wataendelea kumdharau Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said? Watafumua kikosi chao cha utawala wa timu? Watarekebisha mipango yao ya usajili wa timu na kuleta wachezaji wenye hadhi ya Simba katika kikosi? Ni suala la kusubiri kwa sasa..

“Tupo Aprili. Mvua zinanyesha. Tusubiri Aprili ya mwakani kuona Simba itakuwa wapi. Kuona itakuwa imejirekebisha wapi. Leo ni aibu kuona baadhi ya mashabiki wa Simba wakiwa wanapumua baada ya kufungwa na Yanga. Kisa? Eti wamefungwa mabao machache kuliko walivyotazamia. Aibu,” amesema Edo Kumwembe.

SIMBA WASITISHA MAZUNGUMZO YA MIKATABA…MASTAA HAWA HATARINI KUONDOKA…CHAMA ATAJWA MO DEWJI AINGILIA KATI USAJILI SIMBA SC…SEHEMU ZA MABORESHO ZATAJWA…INONGA HATARINI