Home Habari za michezo KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…MABONDIA WAFUNGUKA HAYA…KIDUKU AZIKATAA SIMBA NA YANGA

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…MABONDIA WAFUNGUKA HAYA…KIDUKU AZIKATAA SIMBA NA YANGA

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO...MABONDIA WAFUNGUKA HAYA...KIDUKU AZIKATAA SIMBA NA YANGA

Tangu 1965 ikiwa imepita miaka 59, Simba na Yanga zimekutana mara 111 katika michezo ya watani wa jadi yaani ‘Kariakoo Dabi’.

Katika michezo hiyo, Yanga imeshinda zaidi – mara 39 wakati Simba ikishinda 32 na zimetoka sare mara 40.

Aprili 20, mwaka huu, Simba na Yanga zinacheza mchezo wa 112 tangu zianze kukutana ambapo mchezo wa mwisho msimu huu katika Ligi Kuu Bara, Simba ilikubali kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo ambao ilikuwa mwenyeji kikanuni.

Kwa sasa mchezo wa Karikoo Dabi ndiyo umekuwa gumzo, unaongelewa kila upande na katika kila kundi, na Mwanaspoti limezungumza na mabondia mbalimbali kuelekea katika mchezo huo ambapo kila mmoja amevutia kamba upande wake.

Dullah Mbabe
Bondia Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe ameweka bayana kuwa ni shabiki wa Yanga akisema: “Yanga imekamilika kila idara kuanzia mabeki, washambuliaji hadi viungo ingawa katika michezo ya dabi siku zote huwa haitabiriki sana, lakini kwa upande wangu natamani kuona tunatoa tena kipigo cha bao tano.”

Twaha Kiduku

shabiki wa Azam, lakini kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo huwa hauna mwenyewe na lolote linaweza kutokea ila mtazamo wangu kwa namna upepo ulivyo naona kabisa Yanga anaenda kushinda mchezo huo.”

Mfaume Mfaume
“Siku zote nimekuwa nikisema sina mapenzi ya ushabiki wa hizo timu ila kwa upande wangu naona matokeo ya sare, lakini atakayekuwa amejiandaa vizuri basi anaweza kupata matokeo mazuri ya mchezo huo.

“Lakini ukiniambia juu ya shabiki wa timu gani, basi nitabakia na Taifa Stars kwa sababu mchezaji wa Yanga atacheza, wa Simba, Azam, Namungo, Mtibwa nao watakuwepo humo.”

Ibrahim Class
“Mimi sina ushabiki wa Yanga wala Simba ila kawaida anayeshinda miaka yote ndiyo inakuwa timu yangu japokuwa naona Yanga wanayo nafasi kubwa ya kuweza kupata matokeo ya ushindi kutokana na namna ilivyokuwa bora kwa sasa tofauti na Simba.”

Idd Pialali
“Simba ni timu yangu, lakini ni mkweli kwamba Simba yangu msimu huu ni mbovu na ipo hovyo na kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza mchezo wa Jumamosi kwa kuwa timu yetu ni mbovu na kama watakuwa wametufunga mabao machache, basi yatakuwa mawili ila kama tutajichanganya basi yatakuwa mengine.”

Jesca Mfinganga
“Timu yangu kwanza ni Yanga na naipenda na sina presha kuelekea katika mchezo wa Jumamosi naona kabisa naenda kumchakaza tena mtani wangu kwa kipigo kitakatifu. “Lakini ieleweke kuwa mpira ni kama ngumi ukiweza kujiandaa basi matokeo yanakuwa upande wako ila ukipuuza basi ujue imekula kwako. Naona Yanga akishinda ushindi wa bao 1-0 mpaka 3-0.”

Abeid Zugo
“Kwangu mpira siyo shabiki wake ingawa nawajua wachezaji kama Aziz KI, Mayele na Feisal ambao wameondoka Yanga.

“Lakini ukija kwenye mchezo wenyewe naona utakuwa mgumu kutokana na timu ambazo zinajuana vyema ila naona kabisa Simba inaenda kufungwa tena mabao 5-2.”

Karim Mandonga
“Yanga ni timu yangu halafu naipenda sana. Sina presha juu ya kupata matokeo ya ushindi mbele ya Simba ambayo naona wazi imechoka kulingana na ubora wa Yanga.

“Angalia namna ambavyo ilivyoweza kufanya makubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na hakuna ambaye alitegemea lakini iliweza kuweka rekodi kubwa sana ndiyo maana naona wazi Simba haiwezi kuchomoka maana tutawafunga mabao 3-0.”

Fadhili Majiha

“Mpira kabla ya ngumi ndiyo ulikuwa mchezo wangu na Yanga ndiyo imekuwa klabu yangu ninayoipenda, najua hautakuwa mchezo wa kawaida kwa kuwa ni dabi na hata Simba itajipanga kupata matokeo mazuri baada ya mchezo uliopita kuwafunga mabao 5-1.

“Lakini naona Yanga tunaenda kushinda bila presha yoyote, ushindi wangu nampa Yanga ushindi wa mabao 2-0.”

Selemani Kidunda

“Simba ndiyo timu yangu, nakubali kwamba kwa sasa timu yetu imekuwa mbovu sana lakini ukiangalia kwa upande mwengine kuwa hii ni dabi na kawaida huwa haita-biriki hata kidogo.

“Yanga hawatakiwi kuichukulia poa wala kuipuuza kutokana na kuona wao wapo bora kuliko sisi ila nakuhakikishia tunaenda kushinda mabao 2-0.”

SOMA NA HII  AZAM FC YAVUTA KITASA HICHI KIPYA...KWA BEKI HUYU MJIPANGE...ATAMBA MASHINDANO YA CHAN