Home Uncategorized VITA YA WABABE HAWA NDANI YA LIGI KUU BARA YASIMAMISHWA KWA MUDA

VITA YA WABABE HAWA NDANI YA LIGI KUU BARA YASIMAMISHWA KWA MUDA


LIGI Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kwa muda wa siku 30 ili kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.
Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitangaza Machi 17 kusimamisha masuala yote yanayohusu mjumuiko ya watu ambayo haina ulazima ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya Corona.
Wakati ligi inasimama kasi ya kuwania kiatu cha dhahabu ilikuwa imapamba moto kinara alikuwa ni Meddie Kagere wa Simba ambaye ana mabao 19 vita yake na wakali wenzake tisa itasimama kwa muda mpaka pale itakaporejea upya baada ya hali kuwa salama.
Wababe wengine ambao alikuwa anakimbizana nao kwa kucheka na nyavu ni pamoja na Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar, Reliants Lusajo wa Namungo, Paul Nonga wa Lipuli hawa wametupia mabao 11 kila mmoja.

Bigirimana Blaise, wa Rwanda ametupia mabao 10 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa anakipiga ndani ya Namungo ambaye pacha yake na Lusajo imekubali ndani ya Namungo iliyo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery.

Peter Mapunda, wa Mbeya City amefunga mabao tisa huku
 Daruwesh Saliboko, David Molinga, Ayoub Lyanga wa Coastal Union na Obrey Chirwa wa Azam FC wametupia mabao nanenane kila mmoja.
Mhilu nyota wa Kagera Sugar amesema kuwa kusimamishwa kwa Ligi Kuu Bara ni afya kwa wachezaji kutokana na kupambana na virusi vya Corona kwani ni janga la Taifa.
SOMA NA HII  SABA WA SIMBA KUIKOSA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO DHIDI YA NAMUNGO