Home Michezo MSECHU:- SIMBA WAKIIFUNGA YANGA MNITTE PENDO…AWAPA TAHADHARI HII MASHABIKI WA MSIMBAZI

MSECHU:- SIMBA WAKIIFUNGA YANGA MNITTE PENDO…AWAPA TAHADHARI HII MASHABIKI WA MSIMBAZI

MSECHU:- SIMBA WAKIIFUNGA YANGA MNITTE PENDO...AWAPA TAHADHARI HII MASHABIKI WA MSIMBAZI

Msanii wa Bongo Fleva na msanii maarufu wa Bongo Fleva, Peter Msechu amesema kuwa iwapo kikosi cha Yanga kitafungwa kesho dhidi ya watani wao Simba SC basi abadilishiwe jina badala ya kuitwa Peter aitwe Pendo.

Kesho Yanga wanatarajia kushuka dimbani kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku wakipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na uwezo wao.

“Kwa kifupi ukitaka kupunguza stress na kuwa na maisha marefu duniani, shabiki wa Simba kesho kaa nyumbani kwa sababu unaweza kupaona nyumbani kwako kutoka uwanjani ni kama unaenda mkoani, huo ndio ujumbe wangu.

Kwenda patakuwa karibu lakini kurudi patakuwa ni mbali sana.
“Yani Yanga akifungwa kesho na Simba, mimi si naitwa Peter? Basi niitwe Pendo, basi,” amesema Peter Msechu.

SOMA NA HII  BENCHI LA UFUNDI YANGA LAMBANIA PACOME...ALI KAMWE AMEFUNGUKA HAYA A-Z