Home Habari za michezo TETESI:MZAMIRU KUONDOKA SIMBA…ATIMKIA TIMU HII BONGO…KIBU KUSAINI

TETESI:MZAMIRU KUONDOKA SIMBA…ATIMKIA TIMU HII BONGO…KIBU KUSAINI

Habari za Simba leo

Wakati Simba ikiwa kwenye mapambano ya kuhakikisha Kibu Denis anasaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Msimbazi, kuna tetesi kuwa Mzamiru Yassin yupo kwenye mawindo ya Ihefu na Azam FC.

Inatajwa kuwa tayari Ihefu imewasilisha ofa mezani kwa Mzamiru huku Azam FC ikiwa imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo ambaye amedumu Simba kwa muda mrefu tangu aliposajiliwa akitokea Mtibwa Sugar.

Mkataba wa Mzamiru na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu lakini hadi sasa bado hajaongeza mkataba mwingine, kwa hiyo kama Simba haitamuongezea mkataba mpya huenda akaondoka akiwa mchezaji huru.

SOMA NA HII  BAADA YAPEWA UHAKIKA MSIMBAZI...MGUNDA NI MWENDO WA KUCHEKA TU....AFUNGUKA HAYA KUHUSU MASTAA WAKE..