Home Habari za michezo MZEE MPILI:- NIKO TAYARI FIGO YANGU IUZWE PESA APEWE AZIZI KI ABAKI...

MZEE MPILI:- NIKO TAYARI FIGO YANGU IUZWE PESA APEWE AZIZI KI ABAKI YANGA….

Habari za Yanga

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga, Haji Omary maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa yuko radhi kutoa figo yake iuzwe ili achangie pesa kumbakisha klabuni hapo kiungo mshambuliaji wao, Stephanie Aziz Ki.

Aziz Ki ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu, anatajwa kuwa mpaka sasa bado hajasaini mkapata mpya na huenda akatimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu kwani vilabu kama Mamelodi, Al Ahly, ES Tunis na vingine vingi vimeweka mkwanja mrefu kumgng’oa Jangwani.

“Kuna wakati natamani timu yangu isicheze Klabu Bingwa kwa Masuala kama haya yani Magwiji wa Soka barani Afrika wanapenda sana kutukalia kooni, kiukweli Aziz mpira anaujua ila hio hela anayotaka ni nyingi sana inafika muda natamani kuuza figo ni vile tu wateja hakuna.

“Ushauri wangu kwa Viongozi wa Klabu kama Mchezaji ataendelea kusisitiza kupewa hio hela basi waachane nae, wasifanye maamuzi ya kuiumiza Klabu huenda riziki yetu imeishia hapa,” amesema Mzee Mpili, Mwanachama na Shabiki wa Klabu ya Yanga.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU