Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS…SIMBA YAMTAMBULISHA KELVIN KIJIRI…ACHUKUA NAFASI YA MWENDA & KAPOMBE

BREAKING NEWS…SIMBA YAMTAMBULISHA KELVIN KIJIRI…ACHUKUA NAFASI YA MWENDA & KAPOMBE

HABARI ZA SIMBA- KELVIN KIJIRI

UONGOZI WA SIMBA Umethibitisha kuinasa saini ya mlinzi wa kulia, Kelvin Kijiri kutoka Klabu ya Singida Fountain Gates kwa mkataba wa miaka 2.

Kijiri (24) aliisaidia Singida Fountain Gates (Fountain Gates) kumaliza nafasi ya 11 kwenye ligi msimu 2023/2024 kwa kutoa pasi za magoli (assists) 4 msimu uliopita.

Kelvin Kijiri anatajwa kuwa ndiye mbadala sahihi wa Shomari Kapombe, ni mchezaji mwenye kipaji na kasi amekuwa akitumika kuanzisha mashambulizi kutokea upande wa kulia.

Katika nafasi hiyo ya kulia ilikuwa inakaliwa na wachezaji watatu kabla ya Israel Mwenda kuondoka Simba, kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na Shomari Kapombe.

Kuna David Kameta Duchu mabaye nae inasemekana ameomba kuondoka Simba, ili akatafute changamoto mpya, lakini bado haijafahamika atajiunga na klabu gani.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kiliongea na Soka la Bongo juu ya taarifa hizi kuwa Kelvin Kijiri amesaini mkataba wa miaka miwili na muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa.

“Ni kweli tumemsajili mchezaji huyo ambaye ataungana na mkongwe Shomari Kapombe pamoja na Israel Mwenda ambao tumewaongeza mikataba na David Kameta ‘Duchu’,” kilisema chanzo hicho.

Simba katika dirisha hili la usajili ambalo linaendelea, imesajili mshambuliaji Steven Mukwala ambaye ametoka Asante Kotoko ya Ghana, beki Valentin Nouma akitokea timu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo.

Beki ya kati wamemuongeza Chamou Karaboue na Abdulrazack Mohamed Hamza (23) akitokea klabu ya Supersport United ya Afrika Kusini.

Kwenye eneo la kiungo imemsajili Joshua Mutale, Augustine Okajepha, Debora Mavambo, Jean Charles Ahoua na Yusuf Kagoma hivyo ni wazi imejipanga kutengeneza timu bora kwenye maeneo yote ya uwanja.

Iko wazi Simba hadi sasa imeachana na wachezaji kadhaa akiwemo John Bocco aliyetambulishwa JKT Tanzania, Saidoo Ntibazonkiza, Clatous Chama aliyejiunga na Yanga, Kennedy Juma, Sadio Kanoute anayehusishwa kujiunga na JS Kabyile ya Algeria inayonolewa na Bnechika.

SOMA NA HII  ISHU YA PENATI YA SIMBA KURUDIWA IPO HIVI