Home Habari za Simba Leo KANOUTE ANUKIA ZAIDI JS KABYLE YA BENCHIKA

KANOUTE ANUKIA ZAIDI JS KABYLE YA BENCHIKA

habari za simba Kanoute Putin

KIUNGO mkabaji aliyetemwa na Simba hivi karibuni, Sadio Kanoute ‘Putin’ yupo mbioni kutua klabu ya Ligi Kuu ya Algeria, JS Kabylie.

Inadaiwa kuwa, Kocha Abdelhak Benchikha aliyefanya kazi na Sadio Kanoute wakiwa Msimbazi ndiye aliyetoa pendekezo la kiungo huyo wa kimataifa wa Mali asajiliwe katika timu hiyo.

Duru za kispoti zinadai kwamba mazungumzo ya menejimenti ya mchezaji huyo na JS Kabylie yanaendelea vyema na muda wowote Putin ataungana tena na Benchikha katika timu hiyo.

Putin alisajiliwa na Simba msimu wa 2021/22 pamoja na wachezaji wengine akiwemo Pape Sakho, Duncun Nyoni, Nelson Okwa, Mohammed Outtara lakini wote hao walitemwa MSIMBAZI na kumuacha Kanoute akiendelea kusakata kabumbu.

Alicheza Simba kwa takribani misimu misimu mitatu lakini hakufanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya NBC hata moja, lakini pia Kombe la Shirikisho hajachukua huku rekodi za kujivunia zaidi akiwa nazo kwa kubeba kombe 1 la Mapinduzi, Ngao ya Jamii na Kombe la Muungano.

Pia akiwa Simba amewahi kufunga mabao muhimu kwenye mechi kali na ngumu dhidi ya Al Ahly akiwafunga Kwa Mkapa na Cairo mechi ya AFL.

Sadio Kanoute aliyeachwa Simba msimu wa 2024/25 akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja, lakini walikubaliana na Uongozi wa klabu hiyo kumuachia aende kutafuta changamoto mpya nje ya Tanzania, na sasa anapewa nafasi kubwa zaidi ya kujiunga na kocha aliyewahi kupita Simba pia Abdelhak Benchika.

SADIO KANOUTE

Kuzaliwa: Okt 21, 1996

Mahali: Bamako

Nchi: Mali

Urefu: Mita 1.86

Klabu: Huru

Nafasi: Kiungo Mkabaji

Alikopita: Stade Malien, Al Ahli Benghazi na Simba

SOMA NA HII  ALICHOSEMA ROBERTINHO KUHUSU SARR.....AGUSIA ISHU YA SIMBA....