Home Habari za michezo YANGA KULAMBA BIL 1 YA ZAWADI ZA UBINGWA TU…SIMBA., AZAM MHHHH…..

YANGA KULAMBA BIL 1 YA ZAWADI ZA UBINGWA TU…SIMBA., AZAM MHHHH…..

Habari za Yanga leo

Baada ya Ligi Tanzania Bara 2023/24 kumalizika jana Mei 28, Hiki ndicho kiasi cha pesa watakavyopata Vilabu vyote 16 vilivyoshiriki Ligi Kuu Msimu 2023/24.

Fedha hizi ni Bonus kwa Timu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu 2023/24 kutoka kwa Azam TV ambao ndio wenye haki ya kurusha matangazo ya Televisheni.

Mgawanyo wa Fedha ni kama ifuatavyo;

1. Yanga (Sh 600,000,000)

2. Azam (Sh 300,000,000)

3. Simba (Sh 255,000,000)

4. Coastal Union (Sh 200,000,000)

5. KMC (Sh 65,000,000)

6. Namungo (Sh 60,000,000)

7. Ihefu (Sh 55,000,000)

8. Mashujaa (Sh 50,000,000)

9. Tanzania Prisons (Sh 45,000,000)

10. Kagera Sugar (Sh 40,000,000)

11. Singida FG (Sh 35,000,000)

12. Dodoma Jiji (Sh 30,000,000)

13. JKT Tanzania (Sh 25,000,000)

14. Tabora United (Sh 20,000,000)

15. Geita Gold (Sh 10,000,000)

16. Mtibwa Sugar (Sh 10,000,000)

TIMU YENYE NIDHAMU: (Tsh 20,000,000)

Yanga wamechukua ubingwa msimu huu wakiwa na jumla ya zaidi ya alama 70 ambzo si Simba wala Azam walioweza kuzifikia.

Huu unakuwa ni ubingwa wa 3 mfululizo kwa Yanga toka walipokonya Simba taji hilo msimu wa 2020/21 na unakuwa ubingwa wa 30 kwao toka waanze kushinda taji hilo.

Mbali na Mil 600 kutoka Azam TV, pia Yanga watapewa Mil 100 kutoka NBC , Mil 150 kutoka Sportpesa na wakishinda ubingwa CRDB FA Cup kesho kutwa watapewa Mil 150 hivyo kuifanya Yanga kuvuna zaidi ya Bil 1 .

SOMA NA HII  KISA TP MAZEMBE...NABI APANGA KUPIGA PANGA LA MAANA KWA MASTAA YANGA...ISHU IKO HIVI..