INAELEZWA kwamba moja ya majina ambayo muda wowote kuanzia sasa, yatapewa mkono wa kwaheri katika klabu ya Simba SC, ni jina la Winga mwenye udambwi udambwi mwingi mguuni, Willy Essomba Onana.
Moja ya klabu inayomuhitaji zaidi nyota huyo wa Raia wa Cameoon ni klabu ya Supersport United ya Afrika Kusini ambao wanataka kumchukua kwa ajili ya msimu ujao.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba nyota huyo raia wa Cameroon yuko tayari kuondoka katika timu hiyo baada tu ya msimu huu kumalizika licha ya kubakisha mkataba wake wa mwaka mmoja na kikosi hicho unaoisha mwakani.
Mmoja wa kiongozi wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake alifichua dau ambalo Simba imepewa kutoka kwa timu hiyo ya Afrika ya kusini.