Habari za usajili Simba leo
SIMBA WATANGANZA KUANZA KUTOA THANK YOU.. MZEE WA SALUTI AANZA NA CHAMA, MANULA & KAPOMBE
Abubakar
June 17, 2024
1:14 pm
WAKATI mbao Muda wowote kuanzia sasa, Simba wataanza kutangaza wachezaji ambao wataachana nao, na kutangaza wapya, mashabiki mbalimbali wametoa maoni yao akiwemo shabiki maarufu mzee wa saluti.
Shabiki huyo mwenye aina yake ya kushangilia mfano na ile ya aliyekuwa nyota wa klabu hiyo, Mosses Phiri akifunga anashangilia kwa kupiga saluti, leo ametoa maoni yake juu ya wachezaji anao tamani wapewe mkono wa kwaheri.
“Ukiniuliza Panga la shaba au FAGIO lipite pale msimbazi yaani sipepesi macho”
01. JOBE,JOBE,JOBE ,JOBE
02.FRED MICHAEL KOUBLAN
03.BABACAR SARR
04.SAIDO NTIBAZONKIZA
05.SADIO KANAOUTE
06. INONGA BAKA
07. ONANA ESOMBA
08.KENEDY WILSON JUMAA
“Pia kuna hawa niliowaweka kwenye mabano Wakiondoka Sawa wakibaki sawa vyovyote nakubaliana navyo
(MANULA,KAPOMBE,CHAMA)
“Panga hili lina sababu tatu kuna wachezaji linawapitia kwa kutokujituma uwanjani,kuna wachezaji linawapitia kwa Swala zima la Umri halafu kuna wachezaji linawapitia kwa swala zima La Usaliti na usumbufu kwa Kujiona ni Miungu watu kwenye Club..”
Je wewe shabiki wa Simba una maoni gani kwa wachezaji wa timu yako, ni wapi wanatakiwa kuachwa na wapi wanatakiwa kuendelea kusalia kikosini?
Tayari Simba SC imetoa taarifa ya kwamba mashabiki, wanachama na wapenzi wa soka wakae tayari muda wowote fagio la chuma litapita.
Miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuachwa ni Saidoo Ntibazonkiza, Par Omar Jobe, Sadio Kanoute na wengine.