Home Habari za Usajili Yanga MALIPO YA PRINCE DUBE YAKWAMA…YANGA MBIONI KUMTAMBULISHA

MALIPO YA PRINCE DUBE YAKWAMA…YANGA MBIONI KUMTAMBULISHA

HABARI ZA YANGA

Taarifa za uhakika ni kwamba Prince Dube amelipa kiasi cha dola za Marekani 200,000 (takribani Tsh milioni 522) kwenda kwa Azam FC ili kuwa huru na kutafuta changamoto mpya kwingine.

Prince Dube alifanya malipo hayo siku ya ijumaa jioni wiki iliyopita na kutuma vithibitisho vya malipo kwa uongozi wa Azam, uongozi wa Azam unakiri kupokea vithibitisho vya malipo hayo lakini mpaka sasa bado pesa hiyo haijafika kwenye akaunti ya Azam.

Inaelezwa kwamba Dube alipaswa kulipa kiasi cha $300,000 (Tsh 783) kwa Azam FC ili kuwa huru, baada ya majidiliano ya pande zote mbili wakafikia makubaliano ya $200,000 na ndio yaliyo fanyika. Kwa mantiki hiyo Dube amelipa pesa yote inayo takiwa kulipwa.

Kinacho subiriwa sasa ni kiasi hiko cha pesa kuakisi kwenye akaunti ya Azam fc na kisha klabu kutoa tamko rasmi ya kumaliziana/kuachana na mchezaji huyo.

Prince Dube anahusishwa zaidi na Yanga SC ambao wanaihitaji zaidi saini ya mchezaji huyo. Mzimbambwe huyo amekuwa nje kwa muda mrefu sasa tangu aondoke kwa waajiri wake wa zamani.

Sakata la  mchezaji huyo lilifika hadi kwenye kamati ya usuluhishi ya FIFA, na shauri lao  kusikilizwa ndipo kamati hiyo ilipojiridhisha mchezaji huyo   aliondoka kimakosa hivyo anapaswa kuwalipa fidia ya mkataba wake na Azam FC.

Klabu  ya Azam FC kwa upande wao hawana shida na mchezaji husika,  bali walichokuwa wanakitaka ni malipo ya fidia.

SOMA NA HII  VALENTIN NOUMA AANZA NA TSHABALALA...BALAA LAKE USIPIME