Home Habari za Simba Leo KOCHA MPYA SIMBA KUTAMBULISHWA KESHO…ANATOKA AFRIKA KUSINI

KOCHA MPYA SIMBA KUTAMBULISHWA KESHO…ANATOKA AFRIKA KUSINI

Habari za Simba

KLABU ya Simba SC imepanga hadi kufikia mwishoni mwa wiki iwe ishamtambulisha kocha mkuu wa klabu hiyo, ili kuchuka nafasi ya Abdelhak Benchika aliyeondoka klabuni hapo kwa matatizo ya kifamilia.

Msimu uliopita Simba ilimaliza na Juma Mgunda ambaye alikuwa Kaimu Kocha Mkuu akichukua mikoba ya Mualgeria, Abdelhak Benchikha aliyeondoka mwezi Aprili siku chache baada ya kuchapwa 2-1 na Yanga.

Mgunda alikuwa akisaidiana na Seleman Matola ambapo walipambana na timu hiyo ikashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zilizopo hivi sasa ni kwamba, Mgunda mkataba wake na Simba umemalizika, lakini hata hivyo mipango iliyopo muda mrefu ni kusaka kocha mwingine ambaye ataiongoza timu hiyo msimu ujao watakapoenda kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na ile ya ndani ikiwemo Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho (FA) na Ngao ya Jamii.

Kutokana na hilo, Simba wamepanga kabla ya kufika Ijumaa, wawe wamemtambulisha kocha wao mpya ambaye atakuja kuungana na jeshi lake hilo jijini Dar es Salaam.

Mipango iliyopo ni kwamba kuanzia leo Alhamisi mastaa wataanza kuwasili kambini ili kesho Ijumaa wakutane na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye pia ni Rais wa Heshima wa Klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa ajili ya kuweka mikakati sawa kabla ya kwenda kuanza pre season.

Kocha anayepewa nafasi zaidi ni Msauzi, Steve Komphela ambaye taarifa zilizopo zinabainisha kuwa walifanya naye mawasiliano hapo awali. Wengine watakaoongezeka katika benchi la ufundi ni kocha wa viungo, kocha wa makipa na meneja wa timu ambaye anatajwa kurudishwa kundini Patrick Rweyemamu.

SOMA NA HII  SIMBA CHAP SANA WAWAHI POWER DYNAMO