Home Habari za michezo MO HUSSEIN ATOA NENO…STARS KUSAKA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

MO HUSSEIN ATOA NENO…STARS KUSAKA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

Habari za Michezo leo

Tanzania leo inaingia uwanjani ikitafuta ushindi wa pili kwenye michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 itakapovaana na Zambia.

Tanzania ipo kundi E ikiwa pamoja na Morocco, Niger, Congo na Eritrea ambayo ilijitoa, ikiwa imeshacheza michezo miwili, imeshinda mmoja na kupoteza mmoja ipo nafasi ya nne kwenye msimamo unaoongozwa na Morocco yenye pointi sita.

Ushindi wa Taifa Stars kwenye mchezo huu, utafufua matumaini ya kufuzu kwenye fainali hizo zinazofanyika mwaka 2026 nchini Mexico, Marekani na Canada.

Staa wa Taifa Stars, Mohammed Hussein Tshabalala amewaambia mashabiki kwamba mechi ya leo jioni dhidi ya Zambia katika Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini humu; “haina kujuana na watapambana kwa jasho lao lote.”

Tshabalala amesisitiza kwamba anaamini hakutakuwapo na mabadiliko ya kutisha sana kwenye kikosi cha Zambia na wao kama wachezaji wanajua pakuanzia na wameshaifanyia kazi kubwa mechi hiyo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Staa wa Yanga, Mzambia Kennedy Musonda ni miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuanza leo saa 1:00 jioni ingawa Clatous Chama wa Simba hakuitwa kwenye mechi hiyo iliyobeba matumaini kwa timu zote mbili.

Tanzania na Zambia hazijawahi kufuzu michuano hiyo na sasa zinalingana alama katika kundi hilo, kila moja ikiwa na pointi tatu, ambapo Zambia imecheza mechi tatu ikipoteza mbili na kushinda moja.

Timu hizo tano zote zinawania nafasi moja ya juu ili kufuzu kucheza fainali hizo, ikumbukwe kuwa, katika makundi tisa yaliyopangwa, vinara watafuzu moja kwa moja, wakati washindi wanne bora ‘best loser’ watakaobaki watacheza kwa mfumo wa mtoano na mshindi atashiriki mashindano ya FIFA Play-off kuwania nafasi ya kufuzu.

Katika mechi nane za hivi karibuni timu hizo mbili zilipokutana rekodi zinaonyesha kutoshana nguvu ambapo kila timu imeshinda mara mbili, sare nne na kupoteza mbili.

MSIMAMO WA KUNDI E

                P W D L F A Pts
1.Morocco 2 2  0 0 4 1 6
2.Zambia  3 1  0 2 6 6 3
3.Niger     2 1  0 1 2 2 3
4.Tanzania2 1  0 1 1 2 3
5.Congo   1 0  0 1 2 4 0
6.Eritrea   0 0 0 0 0 0 0

SOMA NA HII  HAWA HAPA WABABE WALIOINGIA NUSU FAINALI...LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2023