Home Uncategorized AZAM FC SASA WAMEHAMIA HUKU, KUANZA LEO KAZI

AZAM FC SASA WAMEHAMIA HUKU, KUANZA LEO KAZI

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Azam FC leo wanatarajia kuanza mazoezi ya kujiandaa kulitetea taji lao hilo.

Azam FC ilitwaa taji la Shirikisho kwa kuichapa Lipuli FC bao 1-0. Inatarajiwa kucheza Januari, 27 Uwanja wa Uhuru na Friends Rangers.

Azam FC itamenyana na Friends Rangers kwenye hatua ya 32 bora na mshindi atapenya hatua ya 16 bora.

Kikosi cha Azam FC kilirejea jana, Januari 23 kutoka Shinyanga ambapo kilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC  na kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shaban Chilunda.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wana morali ya kupambana, mashabiki waendelee kuwapa sapoti.

SOMA NA HII  ISHU YA BALE YAMKASIRISHA RAIS