Home Uncategorized KLOPP ANA MATUMAINI YA KUTOSHA KWA MANE, MJAPAN AKICHAFUA KWA MARA YA...

KLOPP ANA MATUMAINI YA KUTOSHA KWA MANE, MJAPAN AKICHAFUA KWA MARA YA KWANZA


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool ana matumaini kwamba majeruhi aliyopata mshambuliaji wake Sadio Mane sio makubwa sana atarejea Uwanjani hivi karibuni.

Mane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves, Jana, Januari 23, kipindi cha kwanza baada ya kucheza dakika 30 na nafasi yake ilichukuliwa na Takumi Minamino, mshambuliaji mpya wa Liverpool aliyekuwa benchi.

Mchezo dhidi ya Woves unakuwa ni wa kwanza kwa Mjapan Minamino kucheza ndani ya Ligi Kuu England baada ya kumwaga kandarasi ndani ya timu hiyo akitokea Red Bull Salzburg.

Liverpool ilishinda kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mchezo huo ambapo mabao ya Liverpool yalifungwa na Jordan Henderson kwa kichwa dakika ya nane na lilisawazishwa dakika ya 51 na Wolves kupitia kwa Raul Jimenez dakika ya 51 na lile la ushindi likipachikwa na Roberto Firmino kwa Liverpool dakika ya 84.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla ya pointi 64 ikiwa kileleni, ikiwaaacha kwa tofauti ya pointi 16 mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 51 huku Wolves ikiwa nafasi ya 7 na pointi zake 34.
SOMA NA HII  SHEVA: MUNGU AMETENDA MAAJABU NIPO KAMILI GADO