Home Habari za Yanga MWAMNYETO MZAWA ANAYEVUTA MPUNGA MREFU YANGA…MIL 300

MWAMNYETO MZAWA ANAYEVUTA MPUNGA MREFU YANGA…MIL 300

Habari za Yanga- Bakari Mwamnyeto

NAHODHA na beki wa kati wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili wa kuendelea kubakia hapo na mkataba huo Umefanya kuwa Beki ghali zaidi nchini na Afrika Mashariki.

Mkataba huo wa miaka miwili Umefanya nyota huyo avune takribani milioni 300 na mshahara wa takribani milioni 10 Kwa Mujibu wa chanzo Cha ndani kutoka Kwa watu wa karibu wa Beki huyo.

Mwamnyeto ameongeza mkataba huo, baada ya kufikia muafaka mzuri na Uongozi wa timu hiyo, katika dau la usajili na mshahara atakaouchukua ndani ya miaka miwili atakayokuwepo hapo.

Beki huyo alisaini mkataba huo, chini ya Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Andre Mtine na Menejimenti ya Mwamnyeto.

Beki huyo amekuwa akitengeneza ukuta wa Yanga akishirikiana na mabeki wengine wa kati akiwamo Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Dickson Job na Gift Fred, japokuwa mara nyingi alikuwa akianzia benchi kuwapisha wenzake kuanza kikosi cha kwanza.

Kabla ya kutua Yanga mwaka Agosti 2020, Mwamnayeto aliitumikia Coastal kwa misimu miwili akiwa pia kama nahodha akitengeneza ukuta imara kwa kushirikiana na Ibrahim Ame ambaye alisajiliwa na Simba wakati Nondo akitua Yanga.

Awali mchezaji huyo alikuwa anahusishwa zaidi kujiunga na Simba, ambao walikuwa wakimfuatilia mchezaji huyo tangu akiwa Coastal Union, na msimu huu kidogo dili litiki,  lakini Yanga fasta wakashitukia  mchongo.

SOMA NA HII  GSM ATUMIA NJIA YA MO DEWJI YANGA IFUZU MAKUNDI...MASTAA YANGA KULAMBA BINGO NONO...