Home Habari za Yanga Leo YUSUPH KAGOMA ANAITAKA SIMBA…AIGOMEA YANGA

YUSUPH KAGOMA ANAITAKA SIMBA…AIGOMEA YANGA

YUSUPH KAGOMA- SIMBA

IFAHAMIKE kwamba Simba na Yanga wote walikuwa wanaitaka huduma ya Yusuph Kagoma kutoka Singida, ila inaelezwa walioenda mbele ni Yanga kwa kuwasiliana na Mchezaji pamoja na timu yake.

Moja kwa Moja Yusuph Kagoma alipeleka ofa kwa Viongozi wa Singida kuwa anahitaji kujiunga na Yanga makubaliano yakaanza kufanyika.

Mwezi mmoja uliopita, Yanga waliilipa Singida kiasi kinachokadiriwa kuwa ni MILLION 30 za Kitanzania kuinasa saini ya Kagoma, kila kitu kilienda sawa na Kagoma akasaini Yanga ya Jangwani.

Baadae sasa inaelezwa kwamba Simba waliwafuata Singida na ofa kubwa zaidi ya Yanga, pesa walizotoa Simba inafika kiasi cha Milioni 50 za Kitanzania. Wakati huo walimuahidi Kagoma Mshahara mnono na ada nzuri kuliko ile ya Yanga.

Singida kwa weledi mkubwa waliwasihi Simba pamoja na Yusuph Kagoma kuwa tayari wao wamefanya biashara na Yanga na wamesaini kila kitu ikiwemo Mchezaji.

Hivyo wao hawahusiki tena na biashara hiyo bali mwenye mali ni Yanga, wao wana haki zote KUHUSU Yusuph Kagoma.

Kinachoendelea kwa sasa ni Yusuph Kagoma kuvutiwa zaidi na ofa ya Simba ambayo ni kubwa ila bahati mbaya kwake ni kuwa alishasaini Yanga.

Kinachosubiriwa tu ni busara kutoka Yanga kumruhusu mchezaji huyo asajiliwe na Yanga na wao, wamkubalie Yusuph Kagoma awarudishie pesa zao.

Suala hili, linakuwa zito kulingana na mahusiano ya hizi timu mbili yalivyo, Yanga na Simba linapokuja suala la kuuzia mchezaji huwa ni gumu sana, hivyo uwezekano wa Kagoma kujiunga na Simba ni mdogo mno kama tundu la sindano.

SOMA NA HII  AZIZ KI ANATESTI MITAMBO...MKATABA UMEISHA YANGA..KAIZER CHIEFS & MAMELODI ZAHUSISHWA