Home Habari za Simba Leo SIMBA YAFUATA KIFAA…ASANTE KOTOKO…ANAJUA KUFUNGA HUYO

SIMBA YAFUATA KIFAA…ASANTE KOTOKO…ANAJUA KUFUNGA HUYO

STEVE DESE MUKAWALA- SIMBA

INAELEZWA kwamba Mnyama Simba yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mshambuliaji Steven Dese Mukwala kutoka Asante Kotoko ya Ghana, ambaye amecheza kwa mafanikio makubwa sana kwa misimu miwili.

Nyota huyo pia anakipiga kwenye timu ya taifa ya Uganda na kuchukua tuzo ya Mchezaji bora wa Mashabiki nchini Uganda.

Steve Dese Mukwala atawasili Afrika Mashariki kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa kisha atasafiri kuja Dar Es Salaam kusaini kandarasi na Simba, kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya uhakika tayari mchezaji huyo yupo safarini kutoka Ghana kurejea nchini Uganda.

Mchezaji huyo msimu amefunga mabao 12 kwenye Ligi ya Ghana, na kwa mujibu wa Transfermarket dau lake la usajili linafika dola 175,000/= sawa na Tsh Milioni 456.

Timu alizowahi kuchezea hadi sasa ni, Vipers SC, Maroons FC, URA FC zote za Uganda, na Asante Kotoko.

Simba inaendelela kufanya mambo yake chini ya kapeti, huku ukitupia macho zaidi kwenye ukanda wa Afrika Magharib na nchini DR Congo, ili kujaribu kuona namna gani wanaweza kupata wachezaji wazuri.

Mpaka sasa mchezaji aliyesainiwa kutoka DR Congo ni Elie Mpanzu winga, anayetumia mguu wa kushoto na ana sifa ya  kupiga mashuti nje ya 18.

Muda wowote kuanzia sasa, anasubiri tu kukamilisha masuala ya mahitaji yakee,  ikiwemo sehemu ya kuishi hapa Tanzania, na kwa sasa anasubiriwa amalize majukumu yake na timu ya taifa ya DR Congo, mechi za kufuzu kombe la dunia.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO...SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI...ZAGOMBANIWA KWA NJUGU....