Home Uncategorized MWADUI FC YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA KESHO TAIFA

MWADUI FC YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA KESHO TAIFA

UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa unahitaji pointi tatu mbele ya Yanga watakapokutana kesho Uwanja wa Taifa. 

Mwadui FC imetoka kupokea kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini. 

Inakutana na Yanga iliyotoka kushinda mabao 3-1 mbele ya Singida United uliochezwa Uwanja wa Taifa. 

Daud Chakala, meneja wa Mwadui FC amesema kuwa malengo makubwa ya timu yao ni kubaki ndani ya ligi na njia itakayowabakisha ni kushinda.

“Ili timu ibaki ndani ya ligi ni lazima ipate matokeo mazuri na hilo linawezekana kwa kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji anahitaji matokeo. 

“Mashabiki watupe sapoti ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea, hatutaki kucheza playoff tena,”

Mwadui FC ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 35 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67.

SOMA NA HII  SAMATTA AMUIBUIA KOCHA YANGA