Home Habari za Simba Leo AHMEDD ALLY…KUHUSU KIBU WALA HAITUSUMBUI SIMBA.

AHMEDD ALLY…KUHUSU KIBU WALA HAITUSUMBUI SIMBA.

Habari za Simba SC

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kitendo cha utovu wa nidhamu wa mshambuliaji wao, Kibu Denis kutokuwepo kambi hakutathiri mipango ya kocha, Fadlu Davids.

Amesema kitendo cha kutokuwepo kambini hadi sasa ni utoro kambini na watamchukulia hatua za kinidhamu kwa kosa la kutokuwasili kambini kwa ajili ya maandalizo ya msimu wa 2024/25.

Ikumbukwe kwamba mchezaji huyo aliongezewa mkataba na klabu hiyo wa miaka miwili zaidi utakaoisha Juni 2026 na kumplipa stahiki zake za kimkataba.

Ahmed amesema kutokuwepo kwa Kibu hakuathiri program za kocha kwa sababu wamefanya usajili kulingana na mahitaji ya timu kwa kuwa na Joshua Mutale, Steven Mukwala.

“Kibu hadi sasa hajaungana na kikosi cha timu hiyo nchini Misri walipoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa Mashindano.

Tulimuongeza mkataba wa miaka miwili na amesaini kuitumikia Simba, tumemlipa fedha zote na mahitaji yote aliyohitaji. amelipwa kama kondakta fedha alikabidhiwa mkononi na kuondoka, kama taasisi ya Simba hatuna deni na mchezaji bali Simba inamdai utumishi wake,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa baada ya kumaliza kwa ligi alienda Marekani wakampa taarifa ya kambi, kupima afya na safar ya Misri. Baadae aliwaambia hati ya kusafiria imejaa.

“Kweli alirudi nabkufatilia hati yake lakini hakutokea ofisini kwa ajili ya safari, alipotafutwa kwa ajili ya kuleta passport akasema ameenda Kigoma, baada ya hapo zimeanza danadana za hapa na pale, tutaendelea kumtafuta lakini jana tulisikia ameenda nje ya nchi,” amesema Meneja huyo.

Kuhusu kupata timu nje , Ahmed ameeleza kuwa hawafahamu na hilo jambo lingekuwepo angetoa taarifa kwa sababu sera ya Simbi kuruhusu mchezaji akipata malisho mema .

“Tusingweza kumzuia na kumfungulia milango ya kwenda, msimamo wetu kuwa ni mtovu wa nidhamu na tutalishuhurikia hilo kwa kufuata kanuni za Simba kwa matukio kama haya,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS KUANZA KUUSAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA 'WANAWAKE' KWA KUCHEZA NA HAWA....