Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY AFUNGUKA MIPANGO YA KOCHA MPYA SIMBA…FADLU DAVIDS AANZA KAZI.

AHMED ALLY AFUNGUKA MIPANGO YA KOCHA MPYA SIMBA…FADLU DAVIDS AANZA KAZI.

Habari za Simba na Ahmed Ally

KLABU YA SIMBA imeweka wazi mipango ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davis wakiwa nchini humo ni kuataka kucheza michezo mitatu na timu ambazo zitawapa ushindani mkubwa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema licha ya timu kuanza mazoezi jana baada ya kuwasili nchini humo, leo jioni Julai 10 wanaanza ratiba rasmi ya maandalizi kuelekea msimu msimu mpya wa mashindano.

Simba imeingia kambini jana Misri katika jiji la Ismailia kwa ajili ya maandalizi (Pre Seasson) na tayari kocha huyo ameingia nchini humo asubuhi ya leo na jioni kuanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu Bara na kombe la Shirikisho Afrika.

“Leo kundi la pili limewasili nchini Misri akiwemo na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha wetu Fadlu na kuanza rasmi ratiba ya program ya mazoezi ya msimu mpya, mazoezi yatakuwa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni,” amesema Ahmed Ally.

Amesema watafanya mazoezi ya Gym na Uwanjani kwa ajili ya kutafuta utimamu wa mwili wa wachezaji ambao wengi wao wametoka kwenye mapumziko baadae watakuwa na michezo mitatu ya kirafiki.

“Tukiwa nchini humu tutacheza mechi tatu za kirafiki bado timu hazijaweka wazi, kwanza zoezi lililopo kwa kocha wetu anaandaa timu yake, kuwafahamu wachezaji na kuwapa mbinu na ufundi baadae tutacheza mechi hizo,” amesema Meneja huyo.

Wakati huo huo Meneja huyo aliweka wazi suala la utambulisho wa nyota wapya unaendelea lakini leo watakuwa na zoezi la kutoa ‘THANK YOU” kwa wachezaji hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo.

Nyota ambaye anakutana na THANK YOU ni kiungo mkabaji, Babacar Sarr aliyesajiliwa kipindi cha dirisha dogo pamoja na Pa Omary Jobe naye muda wowte anaweza kukutana na neno hilo na Freddy Michael anayesalia ndani ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.

SOMA NA HII  SIMBA SC WAPANGUA JANJA YA WYDAD KUTAKA KUSHITAKI CAF ENDAPO WATAFUNGWA LEO...