Home Habari za Simba Leo SIMBA YAPITA NA HUYU…MRITI WA KAPOMBE

SIMBA YAPITA NA HUYU…MRITI WA KAPOMBE

Habari za Simba, Kelvin Kijiri

SIMBA imegusa kila eneo msimu huu isipokuwa mlinda mlango tu hii ni baada ya kukamilisha usajili wa beki, Kelvin Kijiri kutoka Singida Fountain Gate.

Wanalunyasi hao wamesafisha kikosi chao kilichoshindwa kutwaa mataji kwa misimu miwili mfululizo huku wakisajili damu changa kwa kugusa kila eneo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimefunguka kuwa Kelvin Kijiri amesaini mkataba wa miaka miwili na muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa.

“Ni kweli tumemsajili mchezaji huyo ambaye ataungana na mkongwe Shomari Kapombe pamoja na Israel Mwenda ambao tumewaongeza mikataba na David Kameta ‘Duchu’,” kilisema chanzo hicho.

Simba katika dirisha hili la usajili ambalo linaendelea, imesajili mshambuliaji Steven Mukwala ambaye ametoka Asante Kotoko ya Ghana, beki Valentin Nouma akitokea timu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo.

Beki ya kati wamemuongeza Chamou Karaboue na Abdulrazack Mohamed Hamza (23) akitokea klabu ya Supersport United ya Afrika Kusini.

Kwenye eneo la kiungo imemsajili Joshua Mutale, Augustine Okajepha, Debora Mavambo, Jean Charles Ahoua na Yusuf Kagoma hivyo ni wazi imejipanga kutengeneza timu bora kwenye maeneo yote ya uwanja.

Ikumbukwe kuwa   Simba hadi sasa imeachana na wachezaji kadhaa akiwemo John Bocco aliyetambulishwa JKT Tanzania, Saidoo Ntibazonkiza, Clatous Chama aliyejiunga na Yanga, Kennedy Juma, Sadio Kanoute anayehusishwa kujiunga na JS Kabyile ya Algeria inayonolewa na Bnechika.

SOMA NA HII  KUHUSU KUWAACHA MZAMIRU NA ONYANGO....SIMBA WAIBUKA NA HILI TENA....AHMED ALLY AGUSIA YA MO DEWJI...