Home Habari za Simba Leo ALIYETEMWA SIMBA ATAMBULISHWA JKT TANZANIA…JOHN BOCCO NI MWANAJESHI

ALIYETEMWA SIMBA ATAMBULISHWA JKT TANZANIA…JOHN BOCCO NI MWANAJESHI

HABARI ZA SIMBA, JOHN BOCCO

Simba ilitangaza kuachana na John Bocco kama mchezaji wa kikosi chao katika msimu mpya wa 2024/25 lakini kabla ya msimu wa 2023/24 kuisha tayari Bocco alipewa mikoba ya kuwa kocha mkuu wa Kikosi cha Vijana wa Umri chini ya miaka 17 wa klabu ya Simba.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ameonekana akifanya mazoezi kwenye uwanja wa Meja Generali Isamuhyo akiwa na uzi wa JKT Tanzania tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 akiwa kama mchezaji mpya wa kikosi hicho.

Na hatimaye JKT Tanzania wamemtambulisha John Bocco kama mchezaji wao mpya, kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Sehemu ya taarifa yao ilisomeka ” Ladies and Gentlemen muda wa magoli kipa wa wapinzani kukaa roho juu umefika THE TOP SCORER OF ALL TIME, JOHN RAPHAEL BOCCO IS HERE”

Bocco amesajiliwa na JKT Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Simba kumpa mkono wa kwaheri, licha ya kwamba alipewa majukumu mengine ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Nyota huyo ameachana na Simba na kukubaliana na dili la kurudi kucheza uwanjani.

“Bocco tutampa heshima ya kuwa nahodha. Ndio maana tumemsajili kama kocha mchezaji tunaamini bado ana uwezo uwanjani. Pia ana vitu vya ziada atakavyowasaidia wenzake kuwaongoza,” alisema mmoja wa viongozi wa JKT Tanzania.

Nje na Bocco, wachezaji wengine kama Said Ndemla na David Bryson baada ya kumaliza mikataba ya mkopo wamepewa mikataba mipya, hivyo wataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao.

“Ndemla na Bryson walikuwa wanacheza kwa mkopo kutoka Singida Fountain Gate kwa sasa tumewasainisha mikataba mipya kama wachezaji huru,” amesema.

Mbali na hao mshambuliaji Charles Ilanfya aliyeshuka na Mtibwa Sugar, inaelezwa pia amejiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao. John Bocco alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba chini  ya miaka 17.

SOMA NA HII  MOLOKO NI ZAIDI YA AZIZ KI...WANA YANGA HAWAMPI HESHIMA..ANACHANGIA SANA USHINDI