Home Habari za Yanga Leo YANGA WABADILI GIA ANGANI…HAWAENDI TENA KWA MADIBA

YANGA WABADILI GIA ANGANI…HAWAENDI TENA KWA MADIBA

Habari za Yanga

YANGA wabadilisha gia baada ya kuweka wazi kuwa hawataenda nje ya nchi kuweka kambi, kama ilivyokuwa mipango yao ya awali na kuendelea kusalia Avic Town, jijini Dar Es Slaam.

Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mipango yao ya awali ilikuwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kwa ajili ya maandalizi (Pre Seassons), mambo yamebadilika na wataendelea kusalia Tanzania.

Mipango ya ilikuwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 pamoja na kucheza mechi kulingana na proglamu ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Miguel Gamond.

“Tulikuwa na mipango ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya Pre Seasson, tutabaki Avic Town, tukijiandaa kwa msimu mpya wa mashindano, tunaweza kusafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chief, michuano ya Toyota,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa misimu yote wanayofanya vizuri timu yao inatokea katika kambi hiyo na wanaimani wanapotekea Avic Town, wanafanikiwa katika mipango yao ikiwemo kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani na michuano ya kimataifa kwa kucheza robo fainali.

Kuhusu usajili, Kamwe amesema unaendelea kuboresha kwenye nafasi zilionekana zina mapungufu kwa kufuata ripoti na mapendekezo ya Gamond kuimarisha kikosi cha Yanga kwa ajili ya kuleta watu watakaofanikiwa kwenye mipango yao ya kucheza fainali ya Afrika.

SOMA NA HII  KISA 'MGOLI WA KIBABE' WA FEI TOTO DHIDI YA SIMBA....SHABIKI YANGA AFARIKI KWA KUZIDIWA NA FURAHA....