Home Habari za Yanga Leo YANGA YAMFUATA NABI SOUTH…INJIA HERSI AFUNGUKA MAZITO

YANGA YAMFUATA NABI SOUTH…INJIA HERSI AFUNGUKA MAZITO

Habari za Yanga leo

YANGA SC itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inayonolewa na aliyekuwa kocha wa klabuni hiyo Nasreddine Nabi Julai 28 mwaka huu.

Mchezo huo umepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Toyota uliopo Bloemfontein nchini Afrika Kusini ukiwa ni wa michuano ya kirafiki ya Kombe la Toyota.

Taarifa ya Kaizer imethibitisha uwapo wa mechi hiyo ikieleza: “Kaizer Chiefs watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchuano wa kwanza wa Kombe la Toyota utakaochezwa kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein Julai 28, 2024.”

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, amezungumzia mwaliko huo kwa kusema: “Sisi kama Yanga tunafurahishwa sana na mwaliko huu wa kushiriki katika Kombe la Toyota 2024.

“Mchezo huu unaendeleza uhusiano kati ya timu zetu kubwa mbili barani Afrika ambao ulianza mwaka jana tulipowaalika Kaizer Chiefs kushiriki katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi. Tunafurahia mwaliko huu na tunaahidi kutoa mchezo wa ushindani utakaotusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25.”

Kikosi cha Yanga kimeingia kambini siku ya jana kwa ajili ya kujiandaa na pre-season kikiwa na mastaa wote wapya waliosajiliwa kipindi hiki.

Hadi muda huu, Yanga ilikuwa imewatambulisha wachezaji wapya wanne, Clatous Chama aliyetokea Simba, Prince Dube (Azam), Chadrack Boka (FC Lupopo) na Khomeiny Aboubakar (Ihefu).

Huku wachezaji  wengine wakiongezewa mikataba yao ikiwemo mlinda mlango namba moja Djigui Diarra,  AbdulTwalib Mshery, Nickson Kibabage, Kibwana Shomari, Farid Mussa.

SOMA NA HII  MUDATHIR ATUNUKIWA TUZO... MVP...AUCHO & MUSONDA WAHUSIKA